Blogroll

KWA MAWASILIANO ZAIDI TUWASILIANO KUPITIA BARUA PEPE pallangyorachel@yahoo.com AU NIPIGIE KUPITIA NAMBARI 0715187511

Pages

Saturday, November 23, 2013

MAZEMBE NA CS SFAXIEN NANI KUTWAA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA?


Ikiwa ni wiki moja kamili imepita baada ya kushuhudia timu ya taifa ikitolewa katika harakati za kusaka tiketi ya kucheza kombe la dunia 2014 nchini Brazil kufuatia kichapo cha matokeo ya jumla cha mabao 4-1mbele ya Cameroon, taifa la Tunisia sasa litakuwa likigeuza akili zao kwenye michuano ya vilabu barani Afrika pale ambapo CS Sfaxien ikiwa ni nafasi ya kuwatoa machungu wanachini wa nchi hiyo.

Kocha wa CS Sfaxien Ruud Krol alikuwa katika benchi la ufundi la timu ya taifa ya Carthage Eagles kwa michezo miwili ya playoff dhidi ya Indomitable Lions atalazimika sasa kutupia macho mchezo wa mwisho wa wiki wa vilabu barani Afrika Orange CAF Confederation Cup mchezo wa mkondo wa kwanza dhidi ya TP Mazembe. 

Mazembe watakuwa nchini Tunisia Jumamosi tarehe 23 ambapo kocha wake Patrice Carteron anaamini wenyeji wataanza kwa kupewa nafasi kubwa katika mchezo huo.

 Nahodha wa TP Mazembe Tresor Mputu anasema kikosi kimejiandaa vema kwa kuafanya maandalizi ya kufa mtu katika kambi yao ya mazoezi nchini Ghana kabla ya kuelekea Tunisia. 

Mchezo wa marudiano umepangwa kufanyika Lubumbashi nchin DR Congo Novemba 30 na mshindi mbali ya kutwaa taji hilo pia atapokea dolari za kimarekani US $432 000.

Mshindi pia atacheza dhidi ya mshindi wa klabu bingwa Afrika Al Ahly ya Misri katika mchezo wa Super Cup utakaopigwa nchini Misri mwezi Februari 2014.

No comments:

Post a Comment