Na Andrew Chale
Onesho
la Usiku wa Khanga za Kale 2013, maarufu kama ‘5th Extra Vaa Khanga
Party’ linatarajiwa kufanyika jijini Dar es Salaam usiku wa Novemba 8,
kwenye Hoteli ya Serena na kupambwa na burudani ya nguvu kutoka kwa
bendi ya Mashauzi Classic.
Mwandaaji
wa onesho hilo, Asia Idarous Khamsin, amesema tayari maandalizi yake
yamekamilika na amewasihi wadau kujitokeza kwa wingi katika onesho hilo
la aina yake kujionea mitindo mbalimbali ya khanga.
“Wadau
wa mitindo nchini, watapata burudani na kufurahia mitindo ya khanga
itakayooneshwa kwenye shoo hiyo, hii si ya kukosa kwa mwaka huu,”
amesema Asia Idarous.
Amesema
usiku huo, vazi la Khanga ndilo litakuwa maalumu kwa wadau
watakaohudhuria sambamba na kupinga matumizi ya dawa za kulevya.
Onesho
la Usiku wa Khanga za Kale 2013, ambalo mwaka huu limeandaliwa kwa
ushirikiano wa Asia Idarous Khamsin na Fabak Fashions, linatarajiwa kuwa
na shangwe mbalimbali ikiwamo kushirikisha watu maarufu na mastaa
mbalimbali.
Kuhusu
kiingilio, Idarous alisema kwa viti vya kawaida ni sh 30,000 na viti
maalumu itakuwa ni sh 50,000 na kuongeza kuwa tiketi zimeanza kuuzwa
Fabak Fashions Mikocheni na Gift Shop Serena Hoteli.
Amefafanua
kuwa onesho hilo linafanyika chini ya uwezeshaji wa wadhaminiwa kama
bia ya Redd’s, CXC, Clouds FM, Vayle Spring, Magic FM, Eye View, Amina
Design, Kabile, Voice of America, Origin Unite, Channel Ten, DTV, Times
FM, Michuzi Media Group, Event Light na Miss Tz.
No comments:
Post a Comment