Pages

Tuesday, November 12, 2013

KOCHA AL AHLY AJIVUNIA UBINGWA WA CHAMPIONS LEAGUE.

KOCHA wa klabu ya Al Ahly Mohamed Yousef anajivunia kuwapa furaha mashabiki wa soka wa Misri baada ya kushinda taji la Ligi ya Mabingwa barani Afrika jana. Al Ahly ilinyakuwa taji hilo ambalo litakuwa la nane kwao baada ya kuifunga Orlando Piratesya Afrika Kusini kwa mabao 2-0 hivyo kushinda kwa jumla ya mabao 3-1 katika fainali ya mikondo miwili.Akihojiwa mara baada ya mchezo huo, Yousef amesema hiyo ni mara yake ya kwanza kunyakuwa ubingwa wa michuano hiyo kama kocha hivyo anajivunia lakini anajivunia zaidi kikosi chake ambacho kilipambana mpaka kuhakikisha wanafikia hapo.Kocha huyo pia aliwasifu wapinzani wao Pirates kwa kuonyesha ushindani wa hali ya juu na kudai kuwa walistahili kufika hapo ingawa bahati haikuwa upande wao. Al Ahly wakishangilia ushindi wao wa wa African Champions League.

No comments:

Post a Comment