Pages

Monday, November 25, 2013

KIIZA AONGEZWA KWENYE KIKOSO CHA UGANDA CRENES KINACHOSHIRIKI CECAFA


MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Yanga, Hamis Kiiza ni miongoni mwa wachezaji watatu waliongezwa kwenye kikosi cha Uganda kitakachoshiriki mashindano ya CECAFA yanayotarajiwa kuanza Novemba 27, mwaka huu jijini Nairobi.

Kocha wa Uganda Mulitin ‘Micho’ Sredojevic juzi aliongeza wachezaji watatu wanaocheza soka la kulipwa nje ya Uganda ili kukipa nguvu kikosi hicho ambacho kina wachezaji 20 sasa.

Wachezaji ambao wameongezwa ni Aucho Khalid na Daniel Sserunkuma ambao wanacheza soka lao nchini Kenya katika timu za Tusker FC na Gor Mahia FC pamoja na Hamis Kiiza anayechezea Yanga ya Dar es Salaam.

Awali Micho alisema hatatumia mchezaji ambaye anacheza soka nje ya Uganda kwa sababu anajenga timu itakayoshiriki fainali za mashindano ya Afrika kwa wachezaji wanaocheza ndani yatakayofanyika Afrika Kusini 2014 lakini kwa sasa ameamua kuwaweka ili wasaidie kuleta changamoto katika mashindano ya CECAFA.
Kikosi kamili cha Uganda ni makipa ni Ochan Benjamin, Ismail Watenga na Franco Oringa .

Mabeki ni Julius Ntambi, Nicholas Wadada, Isaac Muleme, Godfrey Walusimbi, Richard Kasagga, Savio Kabugo, Ibrahim Kizza  na  Martin Mpuga.
Viungo ni Khalid Aucho, Geoffrey ' Baba ' Kizito, Said Kyeyune, Joseph Mpande, Brian Majwega  na Vincent Kayizzi

Washambuliaji ni Hamis ' Diego ' Kiiza , Emmanuel Okwi na Dan Sserunkuma  na benchi la ufundi linaundwa na Mulitin ' Micho ' Sredojevic ( Kocha Mkuu ), Kefa Kisala ( kocha msaidizi ) , Fred Kajoba (Kocha wa makipa),  Crispus Muyinda (Meneja wa timu) na Dk Ronald Kisolo pamoja na Media afisa Kenneth Muwanga .

Uganda Cranes ipo kundi C pamoja na Rwanda, Sudan na Eritrea na itaanza kutetea ubingwa wake dhidi ya Rwanda Novemba 29 mwaka huu.

No comments:

Post a Comment