Pages

Sunday, November 17, 2013

KASEBA ACHEZEA KICHAPO CHA KO AUSTARALIA

BONDIA Joseph Kaseba amechezea kichapo cha knoukout (KO) toka kwa bondia Jeremy Van Diemen wa Australia kwenye pambano lililofanyika Metro City, Northbridge nchini Australia.

Akizungumza kupitia kwenye mtandao Kaseba alikiri kupoteza pambano hilo kwa KO katika raundi ya pili na kumwagia sifa mpinzani wake kuwa alikuwa mzuri.

“Ni kweli nimepoteza pambano lakini limenisaidia  nimejifunza mambo mengi kwani nimekuja huku vile vile pia ninafanya utafiti kuhusu filamu yangu ijayo niweze kurekodia huku baadhi ya vipande,”anasema Kaseba
 Nae bondia Jonas Segu aliyeambatana na Joseph Kaseba pia  alipigwa kwa KO na Luke Sharp wa huko Austaralia katika raundi ya tano kwenye pambano la utangulizi la raundi 6.

Michezo ya nchi za nje kwa mabondia imekuwa kama utalii kwani kwa mwaka huu hakuna bondia aliyerudi na ushindi kutokana na viwango vyao kuwa vidogo kimchezo vilevile kukosekana kwa sapoti wanapoenda kushiriki mashindano.

Kaseba alishacheza mapambano saba, alishinda manne, mawili kati yao ni KO,  huku akipigwa matatu kwa KO wakati mpinzani wake naye alishacheza mapambano saba, akashinda matano manne kwa KO na sare ni mawili.

Kaseba ni bingwa wa Kick Boxer wa mabara huku akiwa amefanikiwa kuwa mtayarishaji wa filamu za kimapigano Bongo, akiigiza na kuongoza mapigano katika filamu zake ambazo anazimudu sana, filamu yake ya Bongo Mafia imeteka soko la filamu kwani ni kali na ina sisimua


No comments:

Post a Comment