BONDIA Joseph
Kaseba amechezea kichapo cha knoukout (KO) toka kwa bondia Jeremy Van Diemen
wa Australia kwenye pambano lililofanyika Metro City, Northbridge nchini
Australia.
Akizungumza
kupitia kwenye mtandao Kaseba alikiri kupoteza pambano hilo kwa KO katika
raundi ya pili na kumwagia sifa mpinzani wake kuwa alikuwa mzuri.
“Ni kweli
nimepoteza pambano lakini limenisaidia
nimejifunza mambo mengi kwani nimekuja huku vile vile pia ninafanya
utafiti kuhusu filamu yangu ijayo niweze kurekodia huku baadhi ya
vipande,”anasema Kaseba
Nae
bondia Jonas Segu aliyeambatana na Joseph Kaseba pia alipigwa kwa KO na Luke Sharp wa huko
Austaralia katika raundi ya tano kwenye pambano la utangulizi la raundi 6.
Michezo ya
nchi za nje kwa mabondia imekuwa kama utalii kwani kwa mwaka huu hakuna bondia
aliyerudi na ushindi kutokana na viwango vyao kuwa vidogo kimchezo vilevile kukosekana
kwa sapoti wanapoenda kushiriki mashindano.
Kaseba
alishacheza mapambano saba, alishinda manne, mawili kati yao ni KO, huku akipigwa matatu kwa KO wakati mpinzani
wake naye alishacheza mapambano saba, akashinda matano manne kwa KO na sare ni
mawili.
Kaseba ni
bingwa wa Kick Boxer wa mabara huku akiwa amefanikiwa kuwa mtayarishaji wa
filamu za kimapigano Bongo, akiigiza na kuongoza mapigano katika filamu zake
ambazo anazimudu sana, filamu yake ya Bongo Mafia imeteka soko la filamu kwani
ni kali na ina sisimua
No comments:
Post a Comment