Pages

Sunday, November 24, 2013

KAMPUNI YA USAMBAZAJI WA FILAMU YATOA MSAADA KWA WATOTO WENYE MAHITAJI MAALUM

Msemaji wa Kampuni ya usambazaji wa Filamu ya DJ Marketing and Promoshen, Seraphine Baraka kulia akigawa sabuni za Twiga Soup ambayo nayo inasambazwa na kampuni hiyo kwa watoto wanaoishi katika mazingira magumu wa Shule ya Uhuru Mchanganyiko Dar es salaam mwishoni mwa wiki ilyopita kampuni hiyo imetoa sabuni na baadhi ya nguo kwa watoto hawo
Msemaji wa Kampuni ya usambazaji wa Filamu ya DJ Marketing and Promoshen, Seraphine Baraka kushoto akimkabidhi sabuni aina ya Twiga  inayosambazwa na kampuni hiyo kwa Aisha Omari anaelelewa katika kituo cha Shule ya Uhuru Mchanganyiko Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita
Msemaji wa Kampuni ya usambazaji wa Filamu ya DJ Marketing and Promoshen, Seraphine Baraka kushoto akimkabidhi sabuni aina ya Twiga  inayosambazwa na kampuni hiyo kwa Aisha Omari anaelelewa katika kituo cha Shule ya Uhuru Mchanganyiko Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita
Msemaji wa Kampuni ya usambazaji wa Filamu ya DJ Marketing and Promoshen, Seraphine Baraka kushoto akimkabidhi sabuni aina ya Twiga  inayosambazwa na kampuni hiyo kwa Nassoro Hamisi kulia wengine ni Omari Saiki na Ramadhani Rashidi wanaolelewa katika kituo cha Shule ya Uhuru Mchanganyiko Dar es salaam mwishoni mwa wiki iliyopita

  
Na Mwandishi Wetu
KAMPUNI ya usambazaji wa Filamu nchini Tanzania na bidhaa mbalimbali ya DJ Marketeng and promosheni chini ya mkurugenzi wake Daniel Haule mwishoni mwa wiki iliyopita walitoa msaada wa sabuni ya  unga ya Twiga  ambayo wanazisambaza  na kuwapatia  watoto wanaoishi katika mazingira magumu wa kituo cha Uhuru Mchanganyiko Dar es salaam zawadi.

Mbali na sabuni hizo za twiga walitoa na baadhi ya nguo kwa watoto wanaoishi hapo mkurugrnzi huyo ambaye amewaomba watu mbalimbali kusaidi watu wenye maitaji maalumu kama hawo ambao wengine ni walemavu wa macho

Akielezea historia yake Haule ambaye ni mkurugenzi kwa sasa amesema unajua mie nimelelewa katika mazingila magumu sana kifupi mimi ni mtoto wa mtaani ambapo maisha mengi nimeishi kwenye mitaa nikiwa nalala nje hivyo nimefutika katika kidogo nilicho nacho leo nakula na wenzangu naomba watu wawe na moyo wa kujitoa ili kusaidia maisha ya watoto hawa ili waonge mbele

Nae Msemaji wa Kampuni ya usambazaji wa Filamu ya DJ Marketing and Promoshen, Seraphine Baraka amesema huu ni mwanzo tu wa kujenga mahusiano hivyo tunajipanga ili mradi kila wakati tuwe tunawakumbuka mana maisha haya awajajitakia bali ni mungu ndie muweza wa kila jambo
Kampuni hiyo ambayo kwa sasa inatamba na filamu zake mbili za Dasmila na Trouble Make ambazo zimeshirikisha wasanii mbalimbali wanaotamba katika tasnia hiyo

No comments:

Post a Comment