Pages

Wednesday, November 27, 2013

JOHNNY MULLER ATETEA TAJI LAKE LA UBINGWA WA NDONDI NCHINI AFRICA KUSINI.

Mwana masumbwi Johnny Muller raia wa Afrika Kusini jana Jumanne amefanikiwa kutetea taji lake la uzito wa kati baada ya kumshinda mpinzani wake Vhonani Netshidamboni katika raundi ya pili ya mchezo wa jana usiku 

Mchezo huo uliochezwa huko Emperors Palace karibu na Kempton ambapo Muller alicheza kwa dakika 47 katika raundi hiyo ya pili. 

Muller mwenye uzito wa kilogramu 79.05 alianza mashambulizi ya haraka na makali dhidi ya mpinzani wake Netshidamboni mwenye uzito wa kilogramu 77.25 na kumpeleka chini mapema katika rundi ya ufunguzi.
Netshidamboni,mpinzani wa kwanza wa Muller alirejea kwenye mchezo kwa ajili ya kupata ushindi lakini mapema katika raundi ya pili alimwangusha tena chini na kuibuka mshindi.

No comments:

Post a Comment