Pages

Monday, November 11, 2013

AL AHLY MABINGWA AFRIKA BAADA YA KUIFUNGA ORLANDO PIRATES 2-0


Mohammed AbouTrika kwa mara nyingine tena, ameibeba Al Ahly ya Egypt na kutwaa Ubingwa wa Klabu Barani Afrika baada ya Timu yake kuichapa Orlando Pirates ya Afrika Kusini Bao 2-0 katika Mechi ya Marudiano ya Fainali ya CAF CHAMPIONZ LIGI huko Cairo hii leo. 
Abou Trika, ambae ndie aliefunga Bao walipotoka Sare 1-1 huko Johannesburg na Pirates Wiki iliyopita, leo pia alifunga Bao la kwanza katika Dakika ya 54.
Bao la Pili la Al Ahly lilifungwa na Ahmad Abdel Zaer katika Dakika ya 78.
Al Ahly walimaliza Mechi hii wakiwa Mtu 10 baada ya Sherif Abdul Fadil kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu katika Dakika ya 83 baada Kadi za Njano mbili.
Hii ni mara ya 8 kwa Al Ahly kuwa Mabingwa wa Afrika na Mwezi Desemba wataiwakilisha Afrika huko Nchini Morocco kwenye Mashindano ya FIFA ya Klabu Bingwa Duniani.

No comments:

Post a Comment