Pages

Thursday, October 10, 2013

WAYNE ROONEY ATOBOA LA MOYONI, AFURAHIA KUPANGWA KUCHEZA KAMA MSHAMBULIA


Wayne Rooney ametoboa kwamba hakuwa na furaha Manchester United Msimu uliopita kwa vile alikuwa akichezeshwa nafasi ya Kiungo ambayo hakuipenda lakini sasa, chini ya Meneja David Moyes, anafurahia kuchezeshwa mbele kama Mshambuliaji. Amesema: “Ni wazi utaona uchezaji wangu sasa, nina furaha kwenye Soka langu! Moyes amekuja na ananichezesha mbele na nafurahia. Sikuwa na tatizo kucheza nafasi nyingine lakini mimi ni Fowadi na niliona nastahili kuchezeshwa kwenye nafasi yangu!”
Rooney aliongeza kuwa kuchezeshwa nafasi nyingine kulimfanya avunjike moyo na hilo lilisababisha uchezaji wake uathirike.

Alisema: “Kila Mtu Klabuni alijua wapi nataka kucheza. Labda ntakuwa Kiungo umri ukisogea lakini sikupendelea hapo!”
Kuhusu Mkataba wake na Man United ambao umebakia chini ya Miaka miwili kumalizika, Rooney hakusema waziwazi kama atabakia Klabuni hapo au la lakini alifafanua nini kilitokea mwanzoni mwa Msimu huu ilipovumishwa anataka kuhama
Alizungumza: “Ukweli ni kwamba nilikuwa nimetulia ingawa kwa nje ilionekana si hivyo. Nilishaongea na wahusika Klabuni na tulijua nini tunafanya. Klabu ilifafanua kuhusu hilo. Mke wangu alipata Mtoto mpya na nilikuwa na furaha. Siwezi kusema nilitaka kuondoka au la. Nataka kutilia mkazo Soka langu tu. Tutaona nini kitatokea.”

No comments:

Post a Comment