Manchester
United wanapata bao dakika ya pili baada ya Rooney kuachia shuti kali
na kugonga posti na hatimaye mchezaji wa Real Sociedad Iñigo Martínez
anajifunga kwa kuokolea ndani. mpaka Hafu taimu timu ya Manchester ndio
imeenda ikiongozwa kwa bao hilo la mapema la kujifunga huku United
wakicheza vizuri karibu kipindi chote cha dakika za kipindi cha kwanza.
Kipindi cha pili pamoja na United kukosa nafasi nyingi za kufunga timu
zote zimetoka ya bila kufungana kipindi hicho cha pili, dakika 90
zikimalizika kwa bao hilo moja la kujifunga.

Mchezaji
wa Real Sociedad Inigo Martinez akijifunga hapa baada ya presha kubwa
ya washambuliaji wa United moja wapo aikiwa Rooney na Chicharito
walianzishwa mbele kwa ushambuliaji huo.

Baooo.. Wachezaji wa Manchester United wakishangilia kwa kupongezana apa

Mchezaji
hatari wa Manchester United Wayne Rooney (nyuma) na wa Real Sociedad
Inigo Martinez wakigombea mpira hapa kipindi cha kwanza

Wazee
wazima nao walikuwemo kushoto ni Kocha wa zamani wa Manchester
United Sir Alex Ferguson akiteta na Chief Executive David
Gill....usipime!!

Sehemu
maalumu iliyotengwa eneo la Jukwaa likiwa limetengwa maalum kwa ajili
ya Washabiki 1,400 ambao kazi yao ni kuimba Nyimbo ili kuhamasisha timu
yao ya United.
RATIBA/MATOKEO
Jumatano 23 Oct 2013
Bayer 04 Leverkusen 4 v Shakhtar Donetsk 0
Manchester United 1 v Real Sociedad 0
Real Madrid 2 v Juventus 1
Galatasaray 3 v København 1
RSC Anderlecht 0 v Paris Saint-Germain 5
SL Benfica 1 v Olympiacos FC 1
FC Bayern München 5 v FC Viktoria Plzeň 0
CSKA Moscow 1 v Manchester City 2
Post a Comment