Pages

Thursday, October 24, 2013

TIMU YA TAIFA YA WANAWAKE U-20 IPO TAYARI KUIVAA MSUMBIJI






TIMU ya Taifa ya wasichana waliochini ya miaka 20, jana imeendelea na mazoezi ya kujiandaa na mchezo wa kutafuta kufuzu kombe la dunia dhidi ya Msumbiji utakaochezwa kesho katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mazoezi ya timu hiyo yanafanyika katika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam baada ya kuhamisha kambi iliyokuwa wameweka Pwani kwenye kambi ya JKT Mlandizi.

Akizungumzia mchezo huo, Kocha wa timu ya Taifa ya wanawake, Rogasian Kaijage, alisema timu yake ipo vizuri na anaamini wafanya vyema kwenye mchezo huo licha ya kutopata mechi za kirafiki za kimataifa.

“Timu yangu ipo vizuri na naamini itafanya vema katika mashindano yanayotukabili pia nawaomba watanzania watupe sapoti kwa kufika kwa wingi uwanjani kutushangilia”, alisema Kaijage.

Wachezaji walioko kambini ni Amina Ally, Amina Ramadhan, Amisa Athuman, Anastazia Anthony, Anna Hebron, Belina Julius, Donisia Daniel, Esther Mayala, Fatuma Issa, Gerwa Lugomba, Happiness Lazoni, Harriet Edward, Hellen Maduka, Irene Ndibalema, Jane Cloud, Khadija Hiza na Latifa Salum.

Wengine ni Maimuna Hamis, Mwanaidi Khamis, Najiati Abbas, Neema Paul, Niwael Khalfan, Rehema Abdul, Sabahi Hashim, Sada Ramadhan, Shamimo Hamis, Shelder Boniface, Stumai Abdallah, Tatu Idd, Therese Yona, Violet Nicholas, Vumilia Maarifa, Yulitha Kimbuya na Zena Said. 

Fainali za Dunia za U-20 kwa wanawake zitafanyika mwakani nchini Canada. Iwapo Tanzania itaitoa Msumbiji katika raundi hii, raundi inayofuata itacheza na mshindi kati ya Botswana na Zimbabwe na  ikifanikiwa kupita Tanzania itashiriki kwa mara ya kwanza michuano hiyo ya Kombe la Dunia kwa wasichana.

No comments:

Post a Comment