Pages

Sunday, October 20, 2013

MANCHESTER UNITED 1 v SOUTHAMPTON 1, SARE YAMWONGEZEA MACHUNGU KOCHA MPYA DAVID MOYES!


Kwa mara nyingine tena Manchester United imeandikisha matokeo mabaya kwa kutoka sare nyumbani. Goli lililofngwa na nahodha Adam Lallana dakika moja kabla ya mechi kumalizika, limeiwezesha Southampton kuondoka na alama 1 kwenye uwanja wa Old Trafford. Manchester United imepata goli la kuongoza katika dakika ya 25 ya mchezo. Matokeo hayo ya goli 1-1 ni ya kuvunja moyo kwa mashabiki wa Manchester United ambayo imekwisha funga mechi 2 tu miongoni mwa mechi 7 na sasa iko nyuma ya viongozi wa ligi Arsenal kwa alama 8. Katika matokeo mengine ya mechi zilizochezwa,Chelsea waliinyuka Cardiff magoli 4-1, Everton ikailaza Hull 2-1, Swansea iliichapa Sunderland 4-0 Stoke wakatoka sare bila kufungana na West Brom.

Kocha David Moyes kwa mara nyingi matokeo yakiwa tete na ni baada ya  Southampton kubadilisha matokeo dakika za lala salama jioni hii
 Robin van Persie ndiye aliyefunga bao la pekee kwa United dakika ya 26
Van Persie akijitupa kwa Michael Carrick kwa kupongezwa kwa aina yake

Mzee wa Zamani wa  Manchester United aliyekuwa meneja  Sir Alex Ferguson nae alikuwepo leo Old Trafford

 Wayne Rooney akimpongeza Van Persie wakati wakienda mapunziko

Majanga: Nani akijiuguza pembeni ya uwanja huku akilalamika kwa mwamuzi

Dejan Lovren' akiwasawazishia bao Southampton katika dakika za Majeruhi dakika ya 89 Old Trafford

No comments:

Post a Comment