Pages

Sunday, October 13, 2013

FRIENDS RANGERS YAIFUNGA VILLA SCUAD 2-1 KWENYE MCHEZO WA LIGI DARAJA LA KWANZA




TIMU ya Friends Rangers ya Magomeni jana iliwalaza mapema mashabiki wa Villa Scuad pia ya Magomeni baada ya kuifunga mabao 2-1 katika mchezo wa Ligi daraja la kwanza uliochezwa Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

Mchezo huo ambao ulikuwa na ushindani kwa mashabiki a wachezaji pia kiasi cha kuonyeshana ubabe waziwazi ulishuhudia Friends Rangers wakipata bao dakika ya nne kupitia kwa mshambuliaji Credo Mwaipopo lakini Villa Scuad walifanikiwa kusawazisha bao hilo katika dakika ya 11 kupitia kwa mshambuliaji Daniel Jemadari baada ya kupokea pasi toka kwa Gondwe Andrew.

Baada ya Villa Scud kusawazisha bao hilo Friends Rangers walicharuka na kufanikiwa kuongeza bao la pili kupitia kwa mshambuliajia Khalid Rubagula katika dakika ya 14 baada ya kutokea piga ni kupige kwenye lango la Villa Scuad.

Kipindi cha pili kila timu zilifanya mabadiliko hali iliyozidisha uimara wa kila timu huku ladha ya mchezo ikiondoka kutokana na wachezaji wa Friends Rangers kupoteza muda kwa kujiangusha mara kwa mara na kucheza rafu hali iliyosababisha beki Isihaka Chambuli kuonyeshwa kadi nyekundu katika dakika ya 78 baada ya kumkwatua mshambuliaji wa Villa Scuad Najim Benjamin.

Pia kocha wa Friends Rangers Kheri Mzozo aliondolewa kwenye benchi la ufundi baada ya kuonekana kupinga wazi maamuzi ya mwamuzi Omar Yusuph baada ya kusimama na kwenda hadi kwa mwamuzi wa akiba pamoja na meza kuu na kuanza kulalamika kwa sauti lakini cha kushangazaaskari polisi waliokuwepo uwanjani hapo walishindwa kumwondoa hali iliyoacha maswali mengi kwa mashabiki.

Akizungumza baada ya mchezo kocha wa Villa Scuad, Bakari Idd alimtupia lawama mwamuzi wa mchezo huo kwa kukubali vitendo vya ucheleweshaji muda vilivyokuwa vikionyeshwa na viongozi wa Friends Rangers na wachezaji wao hata pale alipoonyesha muda wa ziada kuwa dakika 4 lakini alitumia dakika mbili tu.

“Mwamuzi kachangia kuharibu mchezo kwani wachezaji wa Friends Rangers walikuwa wanajiangusha na pale huduma inapoitwa  daktari wao alikuwa anawakataza kubebwa na huduma ya kwanza na mwamuzi hakuchukua hatua yoyote”, alisma Idd.


No comments:

Post a Comment