ZIMEBAKI siku 18 tu kabla ya kufanyika kwa mechi ya
watani wa Jadi Simba na Yanga.
Lakini nahodha wa Yanga, Nadir Haroub
'Cannavaro' amesema kuwa hajaona jambo geni kwa mshambuliaji wa Simba, Amis
Tambwe, kwani alishakutana na wachezaji wenye viwango vya kimataifa kama Samuel
Eto’o na Didier Drogba.
Cannavaro ambaye ni beki wa timu hiyo na timu ya
taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' alisema jana mara baada ya kumalizika
kwa mazoezi ya timu yake kwenye Uwanja wa Shule ya Sekondari Loyola kuwa hamuhofii
mchezaji huo kwani kwake anamuona ni mtu wa kawaida.
Alisema kuwa kwake Simba ni timu ya kawaida, kwani
wameshakutana mara nyingi hivyo hana shaka nayo, kwani hata katika mchezo wao
wa mwisho wa kufunga Ligi Kuu msimu uliopita, waliweza kuwafunga mabao 2-0.
"Kwa upande wangu huyo Tambwe simuhofii, kwani
naamini kuwa ni mchezaji wa kawaida tu, hana kiwango cha kutisha na Simba ni
timu kama nyingine, hivyo ushindi ni lazima."
Akizungumzia mechi yao ijayo dhidi ya Mtibwa Sugar,
Cannavaro alisema kuwa wanaendelea kijinoa kwa ajili ya mechi hiyo, lakini
wanaimani kuwa watashinda kwa vile kocha amefanya marekebisho kwa makosa
yaliyojitokeza katika mechi zilizopita.
No comments:
Post a Comment