WACHEZAJI wa
kikosi cha kwanza cha Simba, Henry Joseph na Issa Rashind ‘Baba Ubaya’, wako
fiti asilimia 90, baada ya kukaa benchi kwa majuma kadhaa kutokana na majeraha
yaliyokuwa yanawasumbua na kukosa baadhi ya michezo ya Ligi Kuu.
Akizungumza jana baada mazoezi yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Kinesi, Dar es
Salaam, Daktari wa timu hiyo, Yassin Gembe, alisema jukumu la kuwachezesha
wachezaji hao katika mchezo wa Jumamosi liko mkononi mwa Kocha Mkuu wa kikosi
hicho, Abdallah Kibadeni.
“Wachezaji
hao wamerejea uwanjani leo (jana), wamefanya mazoezi pamoja na wenzao, hivyo
jukumu la kucheza katika mchezo wa Jumamosi liko mikononi mwa kocha Kibadeni,”
alisema Gembe.
Gembe
alisema wachezaji, Abdallah Seseme na Adam Miraji hali zao bado si nzuri na
wataendelea kuwa nje kwa muda wa wiki nne na wanaendelea kuhudumiwa kwa ukaribu
na kufanyishwa mazoezi mepesi.
No comments:
Post a Comment