Pages

Wednesday, September 4, 2013

YONDANI NA CHUJI FITI KUIKABILI MBEYA CITY



MABEKI wa Yanga, Kelvin Yondani, Rajabu Zahir pamoja na kiungo Athumani Idd 'Chuji', wameanza kuleta matumaini katika kikosi cha mabingwa hao watetezi, baada ya juzi kuanza mazoezi mepesi.

Yondani aliumia mguu katika mechi ya Ngao ya Hisani dhidi ya Azam, Chuji aliumia goti katika mechi ya kwanza kwenye michuano ya Ligi Kuu dhidi ya Ashanti United, huku Zahir akiumia paja katika mazoezi.

Wachezaji hao wanatarajiwa kujiunga na wenzao kwa ajili ya maandalizi ya mechi yao ya tatu ya Ligi Kuu dhidi ya Mbeya City, wakati wowote kuanzia leo, kutokana na hali zao kuonekana kuwa zinaridhisha.

Katika mazoezi yaliyofanyika jana kwenye uwanja wa Shule ya Sekondari Loyola, wachezaji hao walionekana kufanya mazoezi mepesi peke yao pembeni mwa uwanja huo.

Katika hatua nyingine, Kocha msaidizi wa timu hiyo, Fredy Minziro, amesema kuwa wana matumaini makubwa kuondoka na ushindi kwenye mechi yao inayofuata dhidi ya Mbeya City, itakayochezwa Septemba 14 katika dimba la uwanja wa Sokoine, jijini Mbeya.

Alisema katika mechi hiyo, ushindi ni lazima ambapo kikosi chao kipo kamili na wanatarajia wachezaji wote watakuwa fiti.
"Tutaendeleza wembe ule ule katika mechi yetu ijayo na kikosi chetu kipo vizuri pamoja na wachezaji wote waliokuwa majeruhi wanaendelea vizuri na tuna imani tutakuwa

No comments:

Post a Comment