KITABU cha maisha ya Jose Mourinho, kimesema kuwa kocha huyo wa Chelsea, alimwaga machozi baada ya David Moyes, kupewa jukumu la kurithi mikoba ya Sir Alex Ferguson.
Mwishoni
mwa wiki Manchester United walipata kipigo cha pili mfululizo katika Ligi Kuu England.
Kwa wale
waliokuwa wakiamini kocha huyo wa zamani wa Everton, Moyes, atafanya vizuri
mwishoni mwa msimu akiwa Old Trafford, wameanza kujiuliza kuhusiana na hali
hiyo itachukua muda gani, baada ya Manchester Unite kupata kipigo cha pili
mfululizo kwenye Ligi Kuu England, tena wakiwa nyumbani dhidi ya West Bromwich
Albion.
Hivyo
imeonyesha wazi kuwa Moyes, ameshindwa kuimudu timu, baada ya mwenyewe kukiri
kuwa amerithi mikoba ya kocha mkubwa na matokeo mabaya huenda yakawandama
zaidi.
Makocha
watano ambao wangepaswa kumrithi Ferguson,
badala ya Moyes ndani ya Old Trafford.
5- Carlo Ancelotti
Kocha
Carlo Ancelotti, aliweka wazi kuwa ataondoka Paris Saint-Germain mwishoni mwa msimu
uliopita na klabu pekee iliyoonyesha dalili ya kumnyemelea ilikuwa ni Real Madrid.
Ancelotti,
ambaye ana historia nzuri ya kuongoza klabu kubwa, ingawa aliwahi kuinoa Chelsea, lakini upendo
wake kwa Blues usingeweza kumfanya akatae ofa ya kuinoa klabu hiyo ya Old
Trafford.
Ukiangalia
jinsi alivyokuwa akifanya kazi AC Milan na PSG, alikuwa akijenga mawasiliano
mazuri na wachezaji wenye majina makubwa, ambao angeweza kuwanasa kwa urahisi
akiwa Manchester United.
4- Jurgen Klopp
Ni mtu
ambaye alikuwa kwenye orodha ya makocha wanaowaniwa kumrithi Fergie, lakini
hakuna mazungumzo yaliyofanyika.
Klopp,
amejijengea jina kubwa kwenye soka kwa kupata mafanikio makubwa, baada ya
kuwabadilisha chipukizi wa Borussia Dortmund na kuwa timu yenye uwezo wa kuleta
ushindani na vikosi vikubwa.
Ni
Mjerumani mwenye macho ya kugundua vipaji na kuvitumia uwanjani, jambo ambalo
limeweza kumpa heshima Ulaya na itashangaza kama
hakuna klabu hata moja kubwa ambayo itakayojaribu kumnasa.
United
walikuwa na nafasi hiyo ya kumpa mikoba ya Fergie kocha huyo, ili apate
changamoto za Ligi Kuu England,
lakini wenyewe waliamua kumpa jukumu hilo
Moyes.
Uhusiano
wa Klopp na wachezaji, lazima wachezaji kadhaa wangemfuta kocha hyo England.
3- Laurent Blanc
Blanc
alikuwa United kama mchezaji na sasa amepewa
jukumu la kumrithi Carlo Ancelotti katika klabu ya Paris Saint-Germain, hivyo
angekuwa mtu sasa kutua Old Trafford.
Kocha
huyo wa Ufaransa, alifanya kazi nzuri alipokabidhiwa kikosi cha Bordeaux na angeweza
kupewa jukumu la kuinoa United.
Blanc,
mwenye umri mdogo wa kuweza kuingoza klabu hiyo ya Old Trafford kwa muda mrefu,
huku akiwa uwezo wa kuiongoza timu kwenye hali yoyote.
2- Pep Guardiola
Wakati
Moyes anapewa jukumu la kuinoa United, tayari Pep Guardiola alikuwa ameshamwaga
wino kwenye klabu ya Bayern Munich.
Lakini,
kama United wangefikiria kumfuata mapema ili aweze kumrithi Sir Alex, wangeweza
kumshawishi na Ligi Kuu England
ndio alikuwa akiitaka, ili kujijengea heshima.
Kocha
huyo mwenye malengo, alifanikiwa
kuifanya klabu ya Barcelona
iliyokuwa na vipaji na kuifanya iweke historia kubwa kwenye soka.
1- Jose Mourinho
Huenda
Mourinho amelia au hakulia kwa kuchaguliwa Moyes badala yake, lakini kuinoa United ni kibarua alichokuwa akikitaka
kwa muda mrefu.
Special
One ni kocha ambaye anapenda mambo yaende anavyotaka yeye na ana njia zake,
lakini jambo la kufurahisha ni kwamba anakuwa na uhakika wa mafanikio na
mataji.
United
walipashwa kumpa kumpa kocha huyo wa Ureno kibarua hicho.
Aba uzoefu wa kunyakua mataji kwenye ligi mbalimbali duniani,
ikiwemo Ligi Kuu England,
Serie A, La Liga na Ureno.
Klabu
hiyo ya Old Trafford kama ingemchukua Mourinho, ungekuwa ni uamuzi sahihi wa
kumrithi Ferguson.
No comments:
Post a Comment