SIMBA
imeendelea kuchanja mbuga baada ya kuichapa JKT Ruvu mabao 2-0, katika mechi ya
Ligi Kuu Tanzania Bara, iliyochezwa jana, kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es
Salaam.
Kwa
matokeo hayo, Simba imezidi kuwaacha watani wao wa jadi Yanga kwa tofauti ya
pointi tano, huku ikiendelea kukaa kileleni kutokana na pointi 14, huku ikiwa
haijafungwa zaidi ya kutoka sare mechi mbili na kushinda mechi nne.
JKT
Ruvu iliyoanza ikiongoza katika msimamo wa ligi hiyo kabla ya Simba, imeshuka
hadi nafasi ya saba kutokana na pointi
tisa sawa na Yanga inayoshika nafasi ya tano huku Azam FC ikipanda hadi nafasi
ya nne kutokana na sare ya bao 1-1 na Tanzania Prisons jana na kuifanya timu
hiyo kufikisha pointi 10 sawa na Coastal Union inayoshika nafasi ya tatu huku
Kagera Sugar inaifuatia Simba, baada ya kujikusanyia pointi 11 na Ruvu Shooting
ikiwa nafasi ya sita kutokana na pointi tisa, huku timu zote zikiwa zimecheza
mechi sita kila moja.
Katika
mechi ya jana, Simba ilikuwa ya kwanza kulifikia lango la JKT Ruvu ikiwa ni
dakika ya saba, baada ya Amis Tambwe kupiga shuti kali akitumia krosi ya Amri
Kiemba, lakini alitokea Shaban Dihile na kuokoa hatari hiyo.
Dakika
ya 17, Abdulhalim Humud alioneshwa kadi ya njano kutokana na kumchezea rafu
mshambuliaji wa JKT Ruvu, Salum Machaku.
Hata
hivyo, JKT Ruvu ilipoteza nafasi ya kufunga katika dakika ya 21, baada ya beki
wa timu hiyo, Stanley Nkomola kupiga krosi iliyomkuta Damas Makwaya na kupiga
shuti ambalo liliokolewa na Kipa wa Simba, Abel Dhaira.
Mechi
hiyo iliyochezeshwa na Mwamuzi, Antony Kayombo kutoka Rukwa, alitoa penalti kwa
Simba dakika ya 24, iliyoonwa na mwamuzi wa pembeni, John Kanyenye, baada ya
beki wa JKT Ruvu, Jamal Said kunawa mpira katika eneo la hatari iliyofungwa na
Tambwe na kumfanya akifikishe mabao saba.
Katika
dakika ya 43, Makwaya aliwatoka mabeki wa Simba na kuachia shuti kali, lakini
kutokana na ushupavu wa Kipa, Abel
Dhaira aliondoa hatari hiyo.
Simba
ilipata bao la pili kupitia kwa Ramadhan Singano ‘Messi’ aliyetokea benchi
kuchukua nafasi ya Kiemba, aliyefunga bao la moja kwa moja baada ya kuunganisha
krosi ya Humud.
JKT
Ruvu walipoteza nafasi ya kufunga baada ya Emmanuel Pius kupiga shuti kali
katika dakika ya 80, lakini Kipa wa Simba, Dhaira aliweza kupangua shuti hilo.
Simba
iliwakilishwa na wachezaji, Abel Dhaira, Haruna Shamte, Adeyoun Seif, Gilbert
Kaze, Joseph Owino, Abdulhalim Humud, Amri Kiemba,
Said Ndemla, Amis Tambwe, Betram Mombeki, na Haruna
Chanongo.
JKT
Ruvu: Shaban Dihile, Damas Makwaya, Stanley Nkomola, Omari Mtaki, Jamal Said,
Nashon Naftal, Alhaji Zege, Emmanuel Swita/ Richard Msenya (dk 58), Bakari
Kondo/Paul Ndauka (dk 78), Salum Mchaku na Emmanuel Pius.
Wakati huo huo, Azam FC imetoka sare ya bao 1-1 na Tanzania
Prisons katika mechi iliyochezwa kwenye Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Bao la Tanzania Prisons lilifungwa na Peter
Michael katika dakika ya 36 na, lilifungwa na Kipre Tchetche
dakika ya 49.
Katika
mechi nyingine iliyochezwa kwenye Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam Ashanti
United imetoka sare ya mabao 2-2 na Mtibwa Sugar.
No comments:
Post a Comment