Pages

Monday, August 26, 2013

WALIONG'ARA SIKU YA KWANZA LIGI KUU ENGLAND



 LONDON, England

LIGI Kuu England ilianza rasmi mwisho wa wiki hii, ambapo ilishuhudiwa vigogo mbalimbali vikiumana ili kusaka pointi tatu muhimu.

Mara baada ya vigogo hivyo kuchuana vikali, tayari imeshaonekana kwamba wataweza kutikisa kwenye michuano hiyo.

Kutokana na uwezo waliouonesha wachezaji hao, wachambuzi wa masuala ya soka nchini England wamejaribu kuangalia kikosi cha wiki kinachoundwa na nyota waliotikisa katika siku ya kwanza ya michuano hiyo.

Wanasema Gabriel
Agbonlahor ambaye kwa sasa ana umri wa miaka 26 na ambaye alisajiliwa msimu uliopita, alikuwa mwiba kwa Arsenal katika mechi hiyo ya Jumamosi.

Wanasema Christian Benteke alikuwa msaada mkubwa kwa Aston  Villa, lakini mapande ambayo alikuwa akitengewa na  Agbonlahor ndiyo yaliyomfanya aonekane kuwa tishio.

Mbali na mchezaji huyo, wachezaji wengine watatu ambao walionekana watakuwa tishio ni pamoja na  Ross Barkley.

 Wanasema kuwa hata wachezaji wenzake wa zamani, Martin Keown na Jamie Carragher vilevile wanamzimia.
Wanasema kwa sasa siri ipo wazi, kiungo huyo wa Everton mwenye umri wa miaka  19, alionesha kila kitu kwenye mchezo dhidi ya  Norwich, likiwamo bao tamu alilofunga.

Wachambuzi hao wanasema mchezaji huyo anaonekana kuwa na kiwango kama alichokuwa nacho  wachezaji,  Paul Gascoigne na  Steven Gerrard.

Wanasema nyota huyo ana uwezo wa kusimama vyema kwenye nafasi ya  kiungo.

2) V ni kwa maana ya Victor
Victor Wanyama ni Mkenya ambaye ametokea katika timu ya Celtic, ambaye naye alifanya vizuri kwenye mechi ambayo timu yake iliibuka na ushindi wa bao  1-0  dhidi ya timu ya West Bromwich.

Kuonekana kwake uwanjani ina maana kwamba kwa sasa kuna wachezaji 100 wa kigeni wanaokipiga Ligi Kuu ya England.

Idadi hiyo imefikiwa ikiwa ni baada ya wiki ya kwanza ya miaka  1992, kuwepo wachezaji nane kutoka mataifa ya kigeni,  lakini kwa sasa ligi hiyo imekuwa ni ya  mataifa mbalimbali.

3) Mata
Kevin de Bruyne anaonekana atakuwa mchezaji ambaye ataleta msisimko kwenye kikosi cha  Chelsea.

Hata hivyo timu haiwezi kukamilika bila kuwepo, Juan Mata.
Mchambuzi huyo wa masuala ya soka anasema kuwa kinara huyo ambaye ni mchezaji bora wa mwaka msimu uliopita  Chelsea ndiye chaguo lake na kwamba wachambuzi hao wanasema watafurahi kuona kocha Jose Mourinho akimtumia vilivyo.

Kwa upande wa Manchester United, kocha wa timu hiyo,  David Moyes, kwanza alimuacha nje ya kikosi chake,  Wilfried Zaha na kuwachezesha wachezaji ambao aliamini wangeweza kuwa na nidhamu na kucheza vizuri.

Lakini hata hivyo, kwa zaidi ya dakika 30 timu yake iliutafuta mpira kwa tochi kabla ya umaliziaji kati ya RVP na Danny Welbeck kuleta kitu tofauti kwa  Swansea.

Mwingine aliyetakata alikuwa ni Tom Hitchcock, ambaye alimfurahisha baba yake kipa wa makocha kwenye timu ya QPR, Kevin.

Katika mchezo huo uliopigwa kwenye uwanja wa Loftus, Tom alifunga bao dakika ya  90 lililoipa ushindi dhidi ya  Ipswich, ikiwa ni muda mfupi akitokea benchi.

“Nilifunga bao kwenye michuanoya Kombe la  FA  wakati nikicheza na  baba lakini siyo kwenye Ligi Kuu,” alikaririwa akisema mchezaji huyo.

Alisema kuwa kutokana na hali hiyo, anaweza kufunga mabao mengi ya ushindi wakati baba yake anapokuwa upande wake.

Kwa upande  wake Kevin Nolan, ambaye alipachika bao lililoipa ushindi  West Ham dhidi ya  Cardiff, naye anatajwa kutakata  kutokana na pasi 16 alizowapa Mark Noble, Joe Cole na  Stewart Downing.

Hata hivyo, inaelezwa kuwa nahodha huyo wa Hammers anatahadharishwa kuwa makini kutokana na kwamba mabao mengi aliyopoteza yanaweza kuifanya timu ikaanza kufanya vibaya.

Nolan anatajwa kuwa nguzo muhimu kwa  kocha,  Sam Allardyce na bao lake kama hilo ndilo lilimfanya kuingia kwenye orodha ya viungo sita bora wanaofunga mabao kwenye histori ya Ligi Kuu ya England.

.Timu ya wiki iliyopendekezwa na wachambuzi hao  ambayo inaweza kutumia mtindo wa
(4-3-3) ni  Mignolet (Liverpool); Whittaker (Norwich), Vidic (Manchester United), Lovren (Southampton), Shaw (Southampton); Delph (Aston Villa), Wanyama (Southampton), Barkley (Everton); Agbonlahor (Aston Villa), Van Persie (Manchester United), Welbeck (Manchester United).

Viungo wanaoongoza kwa ufungaji mabao hadi sasa ni
Frank Lampard-  166
Ryan Giggs 109
Paul Scholes 107
Steven Gerrard 98
Gary Speed 80
Kevin Nola 62
Robert Pires 62
David Beckham 62

No comments:

Post a Comment