Pages

Wednesday, August 14, 2013

UCHAGUZI TFF KUFANYIKA OKTOBA 20, FOMU YA RAIS 500,000


Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) imetoa tangazo la uchaguzi wa Kamati ya mpya ya Utendaji ambao utafanyika Oktoba 20 mwaka huu. Pia Kamati hiyo imetoa tangazo za uchaguzi wa Bodi ya Ligi Kuu ya Tanzania (TPL Board) ambao utafanyika Oktoba 18 mwaka huu.

Akitangaza mchakato huo wa uchaguzi leo (Agosti 14 mwaka huu) jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Kamati hiyo Hamidu Mbwezeleni amesema nafasi zitakazogombewa kwa upande wa TFF ni Rais, Makamu wa Rais na wajumbe 13 wa Kamati ya Utendaji wakiwakilisha kanda mbalimbali.

Fomu kwa wagombea zitatolewa kuanzia Agosti 16 mwaka huu kuanzia saa 3 asubuhi hadi saa 10 kamili jioni kwenye ofizi za TFF. Mwisho wa kuchukua na kurudisha fomu ni Agosti 20 mwaka huu. Fomu kwa nafasi ya Rais ni sh. 500,000, Makamu wa Rais ni sh. 300,000 wakati wajumbe ni sh. 200,000.

Mbwezeleni amesema kwa wale ambao walilipia fomu katika mchakato uliofutwa na wanakusudia kugombea nafasi zilezile walizolipia, hawatalipia tena ada ya fomu husika bali watatakiwa kuambatanisha risiti za malipo wakati wa kurudisha fomu za maombi hayo ili kuthibitisha malipo yao.

Kwa upande wa uchaguzi wa TPL Board, fomu zitaanza kutolewa Agosti 16 hadi 20 mwaka huu, na nafasi zinazogombewa ni Mwenyekiti na Makamu Mwenyekiti ambapo ada ni sh. 200,000 wakati wajumbe wa Bodi ada ni sh. 100,000



Tanzania Football Federation
Affiliated to FIFA, CAF and CECAFA

Karume Memorial Stadium, Uhuru/Shauri Moyo Road
P.O.  Box  1574, Dar es  Salaam, Tanzania     .    Telefax:   + 255-22-2861815
E-mail: tanfootball@tff.or.tz    .   Email: www.tfft.or.tz
 

Na.
TAREHE
SHUGHULI

1.

14/08/2013
Kamati ya Uchaguzi ya TFF kutangaza Uchaguzi wa TFF, nafasi za kugombea na sifa za kugombea uongozi wa TFF.

2.

16/08/2013 – 20/08/2013
Kuchukua Fomu za maombi ya uongozi wa TFF kutoka kwa Katibu wa Kamati ya Uchaguzi ya TFF (Katibu Mkuu wa TFF). Fomu zitatolewa kuanzia saa 3.00 Asubuhi hadi saa 10.00 Alasiri. Mwisho wa kurudisha fomu kwa Katibu Mkuu wa TFF ni Jumanne tarehe 20/08/2013 saa 10:00 Alasiri.

3.

21-23/08/2013
Kamati ya Uchaguzi ya TFF kupitia fomu za waombaji uongozi wa TFF. Kutangaza matokeo ya upitiaji fomu na kuweka wazi kwenye mbao za matangazo majina ya waombaji uongozi wa TFF (23/08/2013).

4.

24-26/08/2013
Kutoa fursa ya pingamizi kwa waombaji uongozi. Mwisho wa kupokea pingamizi ni tarehe 26/01/2013 saa 10:00 Alasiri. Pingamizi ziwasilishwe kwa Katibu Mkuu wa TFF. Pingamizi zizingatie matakwa ya Ibara ya 11(3) ya Kanuni za Uchaguzi.

5.

27/08/2013 – 29/08/2013
Wawekaji Pingamizi na waliowekewa Pingamizi kuitwa mbele ya Kamati ya Uchaguzi ya TFF kutoa utetezi wao kuhusu Pingamizi. Kamati kujadili Pingamizi.

6.

30/08/2013 - 03/09/2013
Usaili na kutangaza matokeo ya pingamizi na ya usaili / Kuwajulisha kwa maandishi wagombea matokeo ya usaili. Kutangaza orodha ya awali ya wagombea.
7.
04 – 06/09/2013
Kamati ya Uchaguzi kupitia Sekretarieti ya TFF kuwasilisha kwenye Kamati ya Maadili ya TFF mashauri yote ya maadili, kwa kujadiliwa na kutolewa maamuzi na Kamati ya Maadili ya TFF.

8.

04 – 06/09/2013
Kutoa fursa ya kukata Rufaa kwenye Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF (TFF Elections Appeal Committee) kwa masuala yasiyo ya Maadili. Rufaa zilizoambatanishwa na ada ya malipo ya Rufaa zitapokelewa na Katibu Mkuu wa TFF. Mwisho wa kupokea Rufaa ni tarehe 06/09/2013 saa 10:00 Alasiri.

9.

07-13/09/2013
Kamati ya Maadili ya TFF kupitia mashauri yote yanayohusu Maadili na kuyatolea uamuzi.

10.

14- 16/09/2013
Kamati ya Maadili ya TFF kutoa matokeo ya maamuzi   ya mashauri ya Maadili kwa Kamati ya Uchaguzi ya TFF na wagombea.
11.
17- 19/09/2013
Kukata Rufaa kwenye Kamati ya Rufaa ya Maadili ya TFF. Mwisho wa kupokea Rufaa ni tarehe 19/09/2013 saa 10:00 Alasiri.

12.

20- 24/09/2013
Kusikiliza Rufaa zilizopelekwa kwenye Kamati ya Rufaa ya Maadili ya TFF na kutolea uamuzi.

13.

25-27 /09/2013
Kamati ya Rufaa ya Maadili ya TFF kuwafahamisha Kamati ya Uchaguzi ya TFF na Wagombea matokeo ya Rufaa zilizosikilizwa na Kamati ya Rufaa ya Maadili.
14.
28/09/2013- 02/10/2013
Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF kusikiliza Rufaa za Uchaguzi kwa masuala yasiyo ya Maadili.

15.

03-04/10/2013
Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF kutangaza na kuwapa taarifa za matokeo ya rufaa wagombea waliokata rufaa (zisizohusu mashauri ya Maadili).  Aidha Kamati ya Uchaguzi ya TFF nayo kufahamishwa matokeo ya rufaa hizo.

16.

05/10/2013
Kutoa orodha ya wagombea wote waliopitishwa    kugombea uongozi wa TFF na kuwataarifu  wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Uchaguzi wa TFF.
17.
06/10/2013- 19/10/2013
Kipindi cha Kampeni kwa wagombea wote.
           18.

20/10/2013

Uchaguzi wa Viongozi wa  TFF.

Text Box:







TANGAZO

UCHAGUZI WA VIONGOZI WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA
(TFF)
14/08/2013

1.                Kamati ya Uchaguzi ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) inawatangazia wananchi wote kuwa Uchaguzi wa viongozi wa TFF utafanyika tarehe 20/10/2013 jijini Dar es salaam. Wale wote wanaopenda kuwania nafasi za uongozi wa TFF wanataarifiwa  kuwa fomu za maombi ya uongozi wa TFF zitatolewa kuanzia tarehe 16 Agosti 2013 hadi tarehe  20 Agosti 2013 katika Ofisi ya Katibu Mkuu wa TFF (Idara ya  Fedha), kuanzia saa 03:00 asubuhi hadi saa 10:00 Alasiri. Mwisho wa kurudisha Fomu ni saa 10:00 Alasiri tarehe 20 Agosti 2013.

2.                Nafasi zinazotangazwa kugombewa ni:

(i)                Rais wa TFF.
(ii)              Makamu wa Rais wa TFF.
(iii)             Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF, nafasi kumi na tatu (13).

3.                Mtu yeyote  anayeomba nafasi ya uongozi katika TFF lazima atimize masharti yafuatayo:

(i)                Awe Raia wa Tanzania.
(ii)              Awe na kiwango cha elimu kisichopungua Kidato cha Nne na cheti cha kuhitimu Elimu ya Sekondari.
(iii)             Awe na uzoefu wa uendeshaji wa Mpira wa Miguu uliothibitishwa wa angalau miaka mitano (5).
(iv)             Asiwe na hatia yoyote ya kosa la jinai na kuhukumiwa kifungo bila ya uchaguzi wa faini.
(v)              Awe na umri wa angalau miaka 25.
(vi)             Awe amewahi kuwa ama mchezaji Mpira wa Miguu, Kocha, Mwamuzi au kushiriki katika uendeshaji wa Mpira wa Miguu katika ngazi ya Taifa, Mkoa, Ligi Kuu au Ligi Daraja la Kwanza.
(vii)            Awe mwadilifu, mwaminifu na mwenye uwezo wa kutekeleza majukumu, wajibu na malengo ya TFF kwa weledi.
(viii)          Mtu anayegombea nafasi ya Rais na Makamu wa Rais wa TFF lazima awe na kiwango cha Elimu kisichopungua Shahada ya Chuo Kikuu na awe na uwezo na haiba ya kuwakilisha TFF ndani na nje ya nchi.

4.                Ada za Fomu za maombi ya uongozi ni hizi zifuatazo:

(i)                Rais wa TFF; Shillingi Laki Tano (Tshs. 500,000/=).
(ii)              Makamu wa Rais wa TFF; Shillingi Laki Tatu (Tshs. 300,000/=).
(iii)             Wajumbe wa Kamati ya Utendaji ya TFF; Shillingi Laki Mbili (Tshs. 200,000/=).
5.                Kwa wale ambao walilipia fomu za kugombea katika mchakato uliofutwa na ambao wanakusudia kugombea nafasi zile zile walizozilipia, hawatalipia tena ada ya fomu husika bali watatakiwa kuambatanisha risiti za malipo wakati wa kurudisha fomu za maombi hayo ili kuthibitisha malipo yao.

6.                Ratiba ya mchakato wa Uchaguzi wa TFF imeainishwa hapa chini:



7.                Uchaguzi wa TFF unafanyika kwa mujibu wa Katiba ya TFF na Kanuni za Uchaguzi za TFF.




Hamidu Mbwezeleni

MWENYEKITI

No comments:

Post a Comment