Pages

Thursday, August 15, 2013

KOCHA RHINO RANGERS AANZA TAMBO BAADA YA KUIFUNGA SC VILLA MABAO 4-1

USHINDI wa Rhino Rangers ya Tabora wa mabao 4-1 dhidi ya Sports Club Villa ya Uganda umempa jeuri kocha wao Sebastian Nkoma na kujigamba kuwa hakuna timu itakayomsumbua kwenye ligi kuu msimu huu.

 Akizungumza na LENZI YA MICHEZO kwa njia ya simu toka Tabora, Seba alisema kuwa kila timu itakayokutana na Rhino Rangers ijiandae kupata kipigo kwani mchezo wao hautofautiani.

“Timu yangu imeifunga SC Villa mabao 4-1 kama hizo timu zinazojiita vigogo wa soka nchini, hivyo timu yangu ni bora wajiandae na vichapo tu”, alijigamba Seba.

Rhino Rangers inayomilikiwa na Jeshi la Wananchi Tanzania, Kanda ya Magharibi,  iliweka kambi katika mikoa ya Shinyanga na Mara na kucheza michezo minne huko na kushinda miwili, sare mmoja na kufungwa mmoja imerudi Tabora ambapo ndio nyumbani.

Kwenye mchezo wao na SC Villa mabao ya Rhino yalifungwa na na Julias Masunga dakika ya 23 na Saad Kipanga aliyefunga dakika ya 41, Ally Ahmed dakika ya 73 na Victor Hagai aliyehitimisha karamu ya mabao dakika ya 85.

Naye Mwenyekiti wa Chama cha Soka Tabora (TAREFA), Yusuph Kitumbo alisema timu ya Rhino imecheza mchezo mzuri na nidhamu imeimarika kwani hata mashabiki wameridhishwa na kiwango cha wachezaji.

Rhino Rangers itafungua dimba na Simba Agosti 24, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ally Hassan Mwinyi , Tabora wakati Yanga watakuwa Taifa wakicheza na Ashanti United.


No comments:

Post a Comment