Pages

Thursday, August 15, 2013

HENRY JOSEPH AMALIZA MKATABA NORWAY ARUDI, AANZA MAZOEZI MSIMBAZI




KIUNGO Mshambuliaji  Henry Joseph Shindika aliyekuwa anacheza soka la kulipwa nchini Norway katika klabu  ya Kongsvinger IL Toppfotball amejea nchini juzi baada ya kumaliza mkataba wake.

Akizungumza na LENZI YA MICHEZO akiwa katika uwanja wa Kinesi alipokuwa akitazama mazoezi ya Simba, ambao ndiyo ilikuwa timu yake akichezea kabla ya kujiunga na soka la kulipwa alisema kuwa yupo nyumbani kwa sasa kwani mkataba wake umamalizika.

“Nimerudi nyumbani baada ya mkataba wangu kumalizika hivyo hapa nimekuja kuwasalimia viongozi wangu na wachezaji pia”, alisema Henry.

Pamoja na majibu yake kutoridhisha, LENZI YA MICHEZO iliendelea kumfuatilia na hatimaye lilimkuta akifanya mazoezi na wekundu hao leo asubuhi hivyo huenda akasajiliwa katika dirisha dogo kwani usajili umeshafungwa.

Henry ambaye alijiunga na Kongsvinger IL Toppfotball Februari, 2009 akitokea klabu ya Simba yenye makao yake katika mtaa wa Msimbazi na aliitwa timu ya taifa kwa mara ya kwanza 2006 na aliichezea michezo 24 na kufunga bao moja tu.

Kiungo huyo ambaye alikuwa akivaa jezi namba mbili akiwa Kongs IL Toppfitball aliifunga mabao mawili katika michezo 74 aliyochezea.


No comments:

Post a Comment