Pages

Tuesday, August 20, 2013

DRFA YAENDESHA SEMINA KWA VILABU VYA LIGI KUU NA DARAJA LA KWANZA






MBUNGE wa Ilala Mussa Azzan Zungu leo amefungua semina kwa klabu za Ligi Kuu na Ligi Daraja la Kwanza Tanzania Bara kwa Mkoa wa Dar es Salaam na kusema uchawi katika mpira hakuna.

Zungu alisema hayo wakati akifungua semina hiyo ya siku moja iliyoandaliwa na Chama cha Mpira wa Miguu Mkoa wa Dar es Salaam (DRFA) iliyofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Alisema mpira unataka maandalizi mpira wa miguu unahitaji maandalizi na pesa na kwamba pia unahitaji ghrama kubwa ili kuuendesha.

“Miaka ya nyuma tulikuwa tukicheza mpira
kienyeji ingawa kulikuwepo na sheria 17, sasa msione wale wanaoshindwa kucheza hawajui, tatizo hawajawekeza na ndio maana washuka madaraja,” alisema.

Zungu pia alitumia fursa hiyo kumpongeza nahodha wa Yanga, Nadir Haroub ‘Cannavaro’ kwa kutojisikia na kuhudhuria semina hiyo licha ya uchovu wa mechi ya jana ya Ngao ya Hisani dhidi ya Azam walioshinda bao 1-0.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa DRFA, Almas Kassongo alisema bado ataendelea kupambana na kutowaangusha wadau wa mpira wa miguu Mkoa wa Dar es Salaam.

“Nipo katika mapamabano ya mpira kwa muda mrefu na nitahakikisha timu mojawapo ya Dar es Salaam inaendelea kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom.


No comments:

Post a Comment