Pages

Tuesday, August 27, 2013

BONDIA WA DUNIA FRANCOIS BOTHA ATUA JIJINI DAR KUMSHUHUDIA CHEKA NA PHIL KESHO KUTWA


Mkurugenzi Msaidizi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Bi.Juliana Yassoda akiwa na Bondia wa Dunia wa uzito wa juu Francois Botha alipowasili katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jijini Dar es salaam kwa ajili ya kuzungumzia masuala ya mchezo wa ndondi utakaofanyika 30 Agosti mwaka huu katika ukumbi wa Diamond.
Bondia wa Dunia wa uzito wa juu Francois Botha akionyesha jinsi ya kupambana kulia ni Yasini Abdalla Rais wa Shirikisho la ndondi nchini ,kushoto ni mdau wa ndondi , uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jijini Dar es salaam.
Bondia wa Dunia wa uzito wa juu Francois Botha akionyesha mmoja ya mkanda alioishinda kwa muuandaaji wa pambano hilo J Msangi,kushoto ni Rais wa Shirikisho la Ndondi Howard Goldberg katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jijini Dar es salaam
Bondia wa Dunia Francois Botha akiwa na muuandaaji wa pambano hilo J Msangi,kushoto ni Rais wa Shirikisho la Ndondi Howard Goldberg katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere leo jijini Dar es salaam.(Picha zote na Lorietha Laurence-Maelezo)

No comments:

Post a Comment