Pages

Monday, June 10, 2013

MSANII MATONYA ASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA UTAPELI

http://www.the-star.co.ke/sites/default/files/styles/node_article/public/images/articles/2013/02/07/106327/5_0.png


  

  Msanii huyu yupo nje kwa  dhamana ya laki nane baada ya kusoto selo kwa masaa kadha katika kituo kikuu cha Polisi  Songea mkoani Ruvuma  kutokana na tuhuma za  utapeli .



Matonya amekamatwa kutokana na kufanya utapeli katika show aliyotakiwa kufanya katika ukumbi wa Jambolee uliyopo manispaa ya Songea mkoani Ruvuma. Baada ya kuja ukumbini akiwa amelewa hali iliyompelekea kushindwa kufanya show na kusababisha hasara katika ukumbi baada ya kufanya fujo ya kuvunja vitu ukumbi hapo, Ndipo waandaaji wa show hiyo walipoamua ifanyike kesho yake na kiingilo kiwe ni  kununua bia .



Wakati huo msanii huyo alitakiwa akafanye show ingine wilaya ya Mbinga ambayo ilikuwa ni sehemu ya mkataba wao lakini hakufanya hivo na matokeo yake akaamua kukata Tiketi kurudi Dar es Salaam , Baada ya kuvuja taarifa hizo walimfata hadi alipo kuwa amefikia nakukuta amehamia sehemu ingine. 



Hatua iliyochukuliwa nikumvizia akiwa amepanda bus ndipo alipokamatwa , Hadi sasa yupo nje ya dhamana ya laki nane na anategemewa kupandishwa kizimbani kesho katika mahakama ya mwanzo iliyopo manispaa ya Songea mkoani Ruvuma kujibu tuhuma hizo ,

 Taarifa zaidi zinakuijia endelea kufatilia katika mtandao wetu 

No comments:

Post a Comment