
Mrembo
Lucy Charles akitabasamu baada ya kuvikwa taji la Redd's miss Kanda ya Ziwa
usiku huu.
Kinyanganyiro cha
kumtafuta mnyange wa Kanda ya Ziwa kwa mwaka 2013, kimeteguliwa usiku huu kwenye
Ukumbi wa Hoteli ya Gold Crest baada ya Mrembo Lucy Charles msomi wa chuo kikuu
cha mtakatifu Augustino, kuwabwaga warembo wengine 17 waliojitokeza.
Mrembo huyo aliwapagawisha mashabiki wa urembo waliofurika katika ukumbi
wa Hotel ya Gold Crest baada ya kujibu swali kwa ustadi lililouliza Ni
changamoto ipi kubwa walionayo vijana wa leo.
Mshindi wa pili katika
shindano hilo ni Eshe Rashid na mshindi wa tatu ni Salsha Isdore

Vinara watatu .katikati ni Lucy Charles mshindi wa Redd's
miss Lake zone 2013, kulia ni Eshe Rashid kutoka Mara na kushoto ni Salsha
Isdore kutoka Geita na wote watatu wanaenda ngazi ya taifa.

Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Januari Yussuf
Makamba(kushoto) na kulia ni Meya wa jiji la Mwanza, Stanslaus Mabula wakiwa ni
wageni rasmi

Furaha ikitanda kwa kila mmoja

Hapa kila mmoja alikuwa na wake wa kumchangua na kila mmoja
akijiuliza swali nani kutwaa taji !!

Jamal Kalumuna kutoka Bukoba akiwa na furaha baada ya
kuwaona warembo jukwaanin

Meza kuu Viongozi mbalimbali

Mwandaaji wa Miss Redd's Lake Zone 2013 akisikiliza neno
kutoka kwa
Mkurugenzi
wa kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga

Mc Kulia akiwa na Mwandaaji ambaye anahusika na Swala zima
na akiwa anatoka Clara Salon & Boutique Bi Clara Mwassa.

Furaha zikapenya kwa Viongozi hawa ambao ndiyo walikuwa
majaji

Umati
wa watu ukimwangalia kwa makini Mashidonge wakati anacheza na Moto usiku
huu

Michuzi
ikimfata alipo!!

Babylove Kalalaa akiwa na nyoka wake jukwaani kuwapagawisha
mashabiki wake.

Naibu Waziri wa Sayansi na Teknolojia, Januari Yussuf
Makamba ilibidi asimame maana ilikuwa kazi kweli kweli na kwa mara ya kwanza
namuona na yeye anachukua kumbukumbu kwenye simu yake.!!

warembo wote wakaitwa !!

Kiongozi wa BHATT ELECTONICS LTD Akiteta baada ya
kuchagua warembo na kuwapatia kazi kwenye ofisi zao. Kumbuka BHATT ni wakala wa
Samsung.

Mkurugenzi wa kamati ya Miss Tanzania, Hashim Lundenga
akijiandaa kuanza kuita 10 Bora hapa

Top Ten hii hapa

Tano Bora

Ommy Dimpoz akitumbuiza

Dadaz wakidata na nyimbo za mkali Ommy Dimpoz

Michael Ross Kutoka Uganda nae akaingia kwa mitindo ya aina
yake!!

Dadaz wakimsonga Michael Ross kutaka kumshusha chini
kucheza nae

kamata kitita chako Mrembo!!!

Zawadi zako hizi!!

ushindi mtamu jamaniiii!

Picha ya pamoja Waandaji na majaji wa Redd's miss Lake zone
2013

Wanyange !!

Post a Comment