Pages

Sunday, June 2, 2013

CBE YATWAA UBINGWA WA POOL TABLE KWA UPANDE WA VYUO VIKUU NCHINI

Timu ya CBE wakishangilia baada ya kukabidhiwa kombe

Abukakar Amri (kulia) ambaye ni nahodha wa CBE akiwa aamini kuwa kombe wanalokabidhiwa na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo (BMT) Dioniz Malinzi ni lao

Liliana Meory (kulia) kwa upande wa mchezaji mmoja toka CBE akikabidhiwa kombe lake baada ya kuibuka bingwa kwa upande wa wanawake 

Said Mohamed (kulia) wa Chuo Kikuu Ruaha (RUCO) akipokea zawadi yake ya ngao toka kwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Dioniz Malinzi. Katikati ni meneja wa Bia ya Safari Oscar Shelukindo


Sehemu ya umati uliofurika

CBE wakiendelea na Mbwembwe zao

Twanga pepeta wakitoa burudani

CHUO Kikuu cha Biashara cha Dar es Salaam (CBE) leo kimetwaa ubingwa wa mashindano ya mchezo wa Pool Table kwa Vyuo Vikuu “Safari Lager Higher  Learning Pool Championships” baada ya kukifunga Chuo Kikuu cha Mzumbe, Tawi la Mbeya kwa mabao 13 kwa 5 kwenye fainali zilizochezwa kwenye Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni.

CBE ambao walikuwa wanauwakilisha mkoa wa Dar es Salaam, walikuwa na uchu wa kuchukua kombe kwani wamekuwa wakiishia nusu fainali kwa miaka mitatu mfululizo.
Kwa matokeo hayo CBE walizawadiwa fedha taslimu 2,500,000 na kombe, huku mshindi wa pili Chuo Kikuu cha Mzumbe akijichukulia 1,500,000.

Nafasi ya tatu ilikwenda kwa Mzumbe ya Morogoro ambao pia walipewa 1,000,000 na nafasi ya nne ilishikwa na Chuo Kikuu cha Mwanza, (SAUT) na kupewa 500,0000
Kwa upande wa mchezaji mmoja mmoja kwa wanawake nafasi ya kwanza kwa Lilian Meory ambaye alipewa fedha taslimu 100,000 na ngao, nafasi ya pili ilichukuliwa na Agness Jacob waChuo Kikuu cha SAUT ambaye alipewa 50,000.

Mchezaji mmoja mmoja kwa upande wa wanaume ilichukuliwa na Said Mohamed wa Chuo Kikuu cha Ruaha (RUCO) na kupewa ngao pamoja na 150,000 huku George Tito wa Chuo Kikuu cha Mzumbe Morogoro akiambulia 100,000.

Akizungumza kabla ya kutoa zawadi mgeni rasmi ambaye alikuwa Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania (BMT) Dioniz Malinzi, alipongeza jitihada za bia ya Safari kwa kuanzisha mashindano hayo ambayo yameanza kuiletea sifa Tanzania kimataifa na kukitaka Chama cha Mchezo wa Pool (TAPA) kuendelea kushirikiana na bia ya Safari katika kuendeleza mchezo huo.

“Kwa kipindi kifupi nilichokaa hapa nimegundua kuwa mashindano haya yameandaliwa vema na nampongeza meneja wa bia ya Safari, Oscar Shelukindo kwa kazi nzuri kwani anekuwa hana mapenzi na michezo asingewekeza kwenye pool table hivyo chama cha Pool mshikeni na mshirikiane nae vema”, alisema Malinzi.
Pia bendi ya African Sttarw, wana kutwanga na kupepeta wametoa burudani safi kiasi cha kuwafanya mashabiki waliofurika Leader kuacha viti vyao na kuungana nao katika kusugua kisigino


Mashindano haya yalianza kutimua vumbi  Mei 4, mwaka huu na yalishirikisha Vyuo Vikuu vya mikoa ya Iringa, Mbeya, Morogoro, Dodoma, Arusha, Kilimanjaro, Mwanza na Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment