Pages

Sunday, June 2, 2013

BRAZIL NA UINGEREZA ZATOSHANA NGUVUBAADA YA KUTOKA SARE YA 2- 2



Kwenye mechi ya Timu za Taifa za Brazil na England mechi ikichezwa leo hii Usiku huko Mjini Rio De Janeiro kwenye Uwanja wa Maracana, ambao Jina lake rasmi ni Estadio Jornalista Mário Filho, ikiwa ni ufunguzi rasmi wa Uwanja huo uliofanyiwa ukarabati mkubwa. Brazil ndio walianza kupata bao kupitia kwa mchezaji wao Fred dakika ya 57 kipindi cha pili huku England wakisawazisha kupitia kwa mchezaji matata wa Arsenal dakika 10 kupita, kupitia Oxlade-Chamberlain dakika ya 67. Baadaye mchezaji hatari wa United Wayne Rooney akikimbiza mpira na kuwatoka mabeki na kupaisha kwenye pembe ya goli upande wa kulia akaifungia timu yake ya Taifa bao la pili katika dakika ya 78.Huku Brazil wakisawazisha pia bao hilo dakika ya 82 kupitia mchezaji Paulinho.
Kwa mara nyingine tena, Maracana itachezwa Fainali ya Kombe la Dunia hapo Mwaka 2014 wakati Brazil watakapokuwa Wenyeji na Uwanja huo utachukua Washabiki 78,838 wote wakiwa wamekaa Vitini.
Mara ya mwisho kwa England kucheza Maracana ilikuwa ni Mwaka 1984 walipocheza Mechi ya Kirafiki na kuifunga Brazil Bao 2-0.
Rooney akipongezwa na wenzake baada ya kufunga bao la pili na kufanya 2-1
Strike: Oxlade-Chamberlain watches his long-range strike in
Oxlade-Chamberlain akiangalia mpira wake alioupiga kwa chini ukiingia nyavuni taratibu
Opener: Fred celebrates his goal
Fred akishangilia baada ya kutupia

Neymar akikimbia na mpira huku akiwa anataka kumtoka Glen Johnson, kushoto, na akikwepa kupitia kwa Theo Walcott upande wa kulia

Wayne Rooney akichuana na Thiago Silva

Mchezaji wa England Frank Lampard akipiga mpira

Theo Walcott akipaa na huku akikimbizwa na Hulk

Wachezaji wa England wakizuia ngome kwa kuweka ukuta kuziba shuti la free kiki inayopigwa na Neymar

kipa wa England na Man City Joe Hart akiokoa mpira kutoka kwa Filipe Luis kwa mikono

Theo Walcott akimkaba Filipeusiku huu.
VIKOSI:
-England
Hart, Johnson (Oxlade-Chamberlain 61), Cahill, Jagielka, Baines (Cole 31) Walcott (Rodwell 83) , Jones, Carrick, Lampard (captain) Milner, Rooney.
Subs: Foster, Lescott, Defoe, McCarthy
Goals: Oxlade-Chamberlain (67), Rooney (78)
-Brazil
Julio Cesar, Dani Alves, Thiago Silva, Luiz, Filipe (Marcelo 45), Luiz Gustavo (Hernanes 45), Paulinho (Bernard 83) Oscar (Lucas Moura 56) Hulk (Fernando 72), Fred, Neymar.
Goals: Fred (57) Paulinho (82)

No comments:

Post a Comment