Pages

Thursday, May 9, 2013

WANAVYOSEMA KUHUSU SIR ALEX FERGUSON


 
BOSI wa Manchester United, Sir Alex Ferguson, anatarajia kustaafu mwishoni mwa msimu huu baada ya miaka 26 ya mafanikio kuongoza timu hiyo ambayo inashiriki Ligi Kuu England.

Ulimwengu wa soka umemmiminia sifa Ferguson wakisema alikuwa kocha bora ambaye ametokea kuishi duniani.

Ferguson mwenye umri wa miaka 71 alidhibitisha uamuzi wake Jumatano asubuhi kwamba safari yake ya kuifundisha Manchester United itafika kikomo mwishoni mwa msimu huu.

Wachezaji wa zamani wa Manchester United Paul Ince na David Beckham walisema kuwa Ferguson aliwafanya kama watoto wake.

PAUL INCE

“Nakumbuka siku ya kwanza nilipoenda Manchester United, nilishindwa kufuzu vipimo vya afya na nikawaza kuwa mpango wangu wa kujiunga na timu hiyo utakuwa umekufa,” alisema Ince. “Hata hivyo, Ferguson alinihali kama motto wake.”

“Kucheza chini yake haikua rahisi. Alikua mtu wa mahitaji mengi. Alikuwa na wakati mzuri na mbaya na wachezaji wengi katika msimu 1992-93, lakini anastahili heshima. Alifanya niwe mchezaji mzuri mwenye kiwango kikubwa.

“Nilipokua Blackburn kama kocha na mambo yakawa hayaendi vizuri, tulicheza na Manchester United Uwanja wa Old Trafford na nilitumia dakika 15 au 20 kwenye ofisi yake.

“Aliniambia: ‘Ushauri pekee ninaoweza kukupa ni usiruhusu wachezaji wakufanye ‘katuni’. Usiwape chochote kwasababu, ukiwapa hata kidogo, watachukua kubwa. Jinsi kiwango chako kinavozidi kupanda unapaswa kuzidi kushikilia msimamo wa ujumbe huu’.”

DAVID BECKHAM

Beckham ambaye alishawahi kuicheza Manchester United chini ya Sir Alex Ferguson alisema kocha huyo raia wa Scotland alifanya mabadiliko makubwa na kuwa na mafanikio katika timu hiyo labda kuliko kocha mwingine.

“Mchango ambao alikuwa nayo kwa timu, wachezaji na mashabiki, sidhani kama kuna mtu mwingine kwenye ulimwengu wa soka ambaye anaweza kuwa na mchango kama huo,kamwe!” alisema Beckham ambaye anaichezea Paris Saint-Germain ya Ufaransa.


VINCENT KOMPANY

“Sir Alex, mmoja kati ya makocha bora wa miaka yote. Baada ya miaka 26 ya mafanikio katika soka, wote tunapaswa kumshukuru kwa mchango wake.”

MICHAEL OWEN

“Bado hainiingii! Manchester United bila Sir Alex Ferguson sihisi ipo sawa. Alikuwa mwanamume haswa ni bora ameamua mwenyewe”

KASPER SCHMEICHEL

 “Ni zaidi ya kuvunjika moyo! Meneja bora ambaye amewahi kuishi! Hakuna swali!”

DANNY SIMPSON

“Wow siamini kama Sir Alex amestaafu. Haionekani kama ni kweli. Yeye ni shujaa na ninaona faraja kusema kwamba nimefanya naye kazi”

ROMELU LUKAKU

“Inasikitisha kuskia kwamba mmoja kati ya mameneja bora amestaafu. Sir Alex alikuwa bingwa wa kweli na shujaa.”

CHELSEA FC

Sisi wote katika Klabu ya Chelsea tunapenda kumtakia Sir Alex Ferguson kila la heri anapostaafu. Amekua mpinzani mzuri kwa miaka 26.”

NEIL LENNON

“Soka haitakuwa kama tulivyozoea bila Sir Alex…ameleta mchango mkubwa sana katika mchezo wa soka… sidhani kama kuna mtu anaweza kumbadili.”

PETER SCHMEICHEL

“Nimesikitishwa, nimeshtuka, nimehuzunika. Sikudhani kama kama hiyo siku itakua leo.”

SEPP BLATTER

“Nimetoka kuskia kwamba Sir Alex Ferguson anastaafu mwishoni mwa msimu huu. Mafanikio yake kwenye soka yanamfanya awe bila pingamizi meneja bora.”

GIUSEPPE ROSSI

“Kazi nzuri! Najivunia kuwahi kufundishwa na Sir Alex Ferguson.”

CRISTIANO RONALDO

“Asante kwa kila kitu bosi.”

No comments:

Post a Comment