Pages

Thursday, May 9, 2013

SIMBA KUFUATA UTARATIBU WA TIMU ZA ULAYA KATIKA UENDESHAJI




Simba Sports Club inapenda kuwataarifu wanachama na mashabiki wake kwamba imeingia makubaliano na Open University Consultancy Bureau (Hapa itafahamika kama “OCB”) kwa ajili ya kuandaa mpango mkakati wa klabu (strategic plan).

Mchakato huo unaanza mara moja na OCB wameshaandaa timu yao inayoongozwa na makamu mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania Prof. Tolly Mbwette ambapo ili kufanikisha hilo imebidi kuunda kamati ya marejeo ya Simba SC (Referral committee) ambayo kazi yake kubwa itakuwa ni kuiongoza OCB :-

1. Kuhusu makundi/watu/maeneo yatakayotumiwa kufanya utafiti.
2.  Kunyambulisha kitaalamu nguvu, mianya na maeneo ya maboresho ya mfumo mzima wa Simba SC (SWOT analysis)
3. Kupitia mpango mkakati ukishaandaliwa baada ya kukusanya maoni ya wanachama, wadau na mashabiki wa klabu kabla ya kuupeleka katika kamati ya utendaji kwa kupitishwa ili ukapitishwe na mkutano mkuu wa wanachama.

Katika kikao cha kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club kilichofanyika tarehe 8/5/2013   Referal Committee ya Simba Sports Club iliyochaguliwa ni:-

1. Joseph Itang’are
2. Swedy Mkwabi
3. Francis Waya
4. Ramesh Patel
5. Evance Aveva
6. Mulamu Ng’hambi
7. Salim Mhene
8. Mtemi Ramadhani
9. Moses Basena
10. Henry Tandau
11. Omary Gumbo
12. Michael Wambura
13. Glory Nghayomah
14. Crensencius Magori
15. Honest Njau
16. Ruge Mtahaba
17. Evodius Mtawala
18. Dr Mwafyenga

Kikao cha kwanza kati ya OCB na Kamati husika kitakuwa siku ya tarehe 25/5/2013.
Uongozi wa Simba Sports Club unawataarifu wanachama na wadau kwamba, mpango mkakati huu ndio mwanzo wa mabadiliko ya klabu kuelekea katika kujiendesha kiweledi (professionalism) kwani utabainisha malengo ya klabu kwa kipindi maalumu yakiwemo masuala muhimu kama ujenzi wa uwanja, academy set up, miundo mbinu ya klabu, masuala ya biashara za klabu yakilenga kukuza taswira (brand) ili kufanikisha mauzo ya bidhaa zenye nembo ya klabu, malengo ya mafanikio ya ndani ya uwanja, kujiwekea kiwango/kipimo cha utendaji wa klabu na wanachama (brand goodwill) ili kuvutia wawekezaji.
Mpango mkakati huo pamoja na hayo pia utaweka mipango hiyo katika uhalisia wa utekelezaji na muda wa kutekeleza masuala hayo, jambo litakalofanikisha kuleta kipimo cha utendaji wa uongozi na watendaji wa klabu katika uwajibikaji kwa wadau na wanachama wa klabu.
Mpango mkakati huo utakuwa tiyari kwa ajili ya kuingizwa katika mkutano mkuu wa klabu wa mwaka 2013/2014.

Imetolewa na
Evodius Mtawala
Katibu Mkuu,
 Simba Sports Club.
9/5/2013

No comments:

Post a Comment