Pages

Thursday, May 30, 2013

TWANGA PEPETA KUPAMBA FAINALI ZA POOL TABLE TAIFA

Meneja wa Bia ya Safari, Oscar Shelukindo akifafanua jambo kuhusu fainali za Pool 
Lwiza Mbutu akizungumza na waandishi wa habari. 
 Mchezaji wa Single wa Chuo cha CBE, Liliani Meori 
 Katibu wa Chama cha Pool Taifa (TAPA), Amos Kafwinga akizungumza wakati wa mkutano huo.
 Kiongozi wa bendi ya Twanga Pepeta, Lwiza Mbutu akionesha manjonjo yake wakati wa mkutano na waandishi wa habari leo. Kushoto ni Rapa wa bendi hiyo, Jumainn Said.


BENDI ya Muziki wa Dansi ya Twanga Pepeta, inatarajia kupamba fainali za Michuano ya mchezo wa Pool ngazi ya Taifa yajulikanayo kama 'Safari Lager Higher Learning Competition 2013'.
Fainali hizo zinatarajiwa kupigwa katika viwanja vya Leaders kuanzia jumamosi mpaka Jumapili ambapo anatarajiwa kupatikana bingwa wa michuano hiyo iliyoanza kutimua vumbi Mei 5 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Meneja wa Bia ya Safari Lager ambao ni wadhamini wakuu wa shindano hilo, Oscar Shelukindo alisema, wameamua kuichukua bendi ya Twanga ili kutoa burudani wakati wa fainali hiyo ambayo pia itapabwa na nyama choma kutoka katika bar tano zilizoshinda katika shindano la nyama choma mwaka huu.

Shelukindo alisema, bingwa katika shindano hilo atajinyakulia kitita cha sh mil 2.5 pamoja na kombe huku zawadi nyingine zikitolewa kwa mshindi wa pili na mchezaji mmoja mmoja na kudai kuwa, timu nane zitachuano ambao ni mabingwa wa kila Mkoa.

Nae Kiongozi wa bendi ya Twanga Luiza Mbutu alisema, wamejipanga kufanya burudani kali ikiwa ni pamoja na kuwatambulisha wapenzi na mashabiki wao nyimbo mpya na kuwataka kuja kwa wingi kwani hakuna kiingilio.
Katika fainali hizo bingwa mtetezi ni chuo cha Sauti Mwanza ambacho pia kimefanikiwa kuingia katika kinyanyang’anyiro hicho mwaka huu.

No comments:

Post a Comment