Pages

Thursday, May 2, 2013

TIGO YAJA NA HUDUMA YA TWITTER YA KUKUWEZESHA KUCHAT LIVE NA CELEBRITY UMPENDAYE NA KUMWULIZA MASWALI KADRI UPENDAVYO NA YEYE KUKUJIBU PAPO HAPO


KAMPUNI ya simu za mikoni ya tigo juzi imezindua huduma ya ukurasa wake mpya wa Twitter wa kuchati moja kwa moja, huduma ambayo ni ya kipekee na ya kwanza Tanzania.
Wapenzi wa Tigo Twitter wanaweza kuchati na mastaa wawapendao moja kwa moja kwa njia ya mtandao huo kwa muda wa saa nzima na msanii Elias Barnaba amepewa nafasi ya kuchati na mashabiki wake  moja kwa moja pia wanaweza kumuuliza maswali ambapo atayajibu papo hapo.
Akizungumza na waandishi wa habari Meneja Chapa wa Tigo,  William Mpinga alisema kuwa wanajivunia kuwapa wapenzi wa tigo Twitter jukwaa la kuonana na kubadilishana nao uzoefu wa maisha na kupitia huduma hii ya kipekee.
“Tigo inajivunia kuwapa wapenzi wa Tigo Twitter jukwaa la kuonana na kuchati moja kwa moja na mastaa wawapendao kupitia ‘Twitter Celeb Live Chat’, ambapo wataweza kufurahia na kubadilishiana nao uzoefu wa maisha”, alisema Mpinga
Hivi karibuni, Tigo Tanzania ilipata tuzo ya utambuzi ya dunia kwa kuwa kampuni pekee inayowasiliana na wateja wao moja kwa moja kupitia kurasa za mtandao mbalimbali ya kijamii kama Facebookiliyotolewa na shirika la SocialBakers,Februari 7, mwaka huu.
Ili kushiriki katika huduma hii ya kuchati moja kwa moja unahitaji kuungana na Tigo Tanzania kupitia mtandao wa kijamii wa Twitter, kisha tumia #OngeanaTigoCeleb na weka Tigo using @Tigo_Tz @jina la celeb.
Kama haujajiunga na mtandao wa Twitter, tafadhali tumia hatua rahisi zifuatazo ili kuweza kunufaika huduma hii bomba ya Tigo: Andika @Tigo_Tz kwenye search kisha bofya, utatokea ukurasa wa Tigo. Bonyeza kwenye follow. Baada ya hapo rudi kwenye ukurasa wako wa Twitter na utaweza kuziona Tweet za Tigo na celeb.
          KUHUSU TIGO:
Tigo ni mtandao wa kwanza wa simu za mkononi nchini Tanzania. Ilianza shughuli mwaka 1994 na inapatikana katika mikoa ishirini na sita (26)
Tanzania bara na visiwani.

Lengo la Tigo ni kuwa mtandao unaoongoza kwa kutoa huduma bora na za ubunifu Tanzania kwa wateja wake wote ambazo zinaendana na mahitaji yao kuanzia huduma za sauti za bei nafuu, vifurushi vya intaneti vyenye kasi kubwa na huduma bora za fedha za simu za mkononi kupitia Tigo Pesa.

Tigo ni sehemu ya kampuni kubwa ya <http://www.millicom.com/> Millicom
International Cellular S.A (MIC) ambayo ni ya unafuu wa huduma na inapatikana kirahisi  kwa zaidi ya wateja milioni 43 katika masoko 13 barani
Afrika na Amerika ya Kusini.                                                                                       

No comments:

Post a Comment