Pages

Thursday, May 9, 2013

SIR ALEX FERGUSON ALIMWAGA MACHOZI WAKATI ANAWAAMBIA WACHEZAJI WAKE KUSTAAFU KUWAFUNDISHA!



Sir Alex anatajwa kuwa ndiye meneja mwenye mafanikio makubwa katika historia ya soka la Uingereza.
Mabingwa wa Ligi Kuu nchini England, Manchester United wametangaza kwamba, Sir Alex Ferguson atastaafu kama meneja wa klabu hiyo mwishoni mwa msimu huu.

Tangu alipojiunga na klabu hiyo mnamo mwaka 1986, ameshinda mataji mawili (2) ya Klabu Bingwa Barani Ulaya, mataji kumi na tatu(13) ya Ligi Kuu ya England na Kombe la FA mara tano(5).

Katika taarifa yake, Sir Alex amesema ni muda muafaka kwake kustaafu wakati klabu ikiwa imejizatiti katika nafasi nzuri.
Ferguson atabakia Manchester United kama mmoja wa wakurugenzi na balozi.

Watu mbalimbali wamekuwa wakitoa salamu za kumtakia kheri, miongoni mwao akiwemo Waziri Mkuu wa Uingereza,David Cameron na wanasiasa mbalimbali pamoja na mashabiki na wachezaji wa zamani wa Uingereza na Manchester United. 

Hofu imetanda miongoni mwa mashabiki wa Manchester United ambao wamekuwa wakijiuliza maisha yatakuwaje bila ya Sir Alex Ferguson kwenye klabu hiyo yenye mashabiki wengi Ulimwenguni.


MAFANIKIO YA ALEX FERGUSON
MATAJI 49 YA FERGIE…
Sir Alex Ferguson ameshinda mataji 49 akiwa kocha mwenye mafanikio zaidi Uingereza…
ST MIRREN
Daraja la Kwanza Scotland (1): 1976-77.
ABERDEEN
Ligi Kuu Scotland (3): 1979-80, 1983-84, 1984-85.
Kombe la Scotland (4): 1981-82, 1982-83, 1983-84, 1985-86.
Kombe la Ligi Scotland (1): 1985-86.
Kombe la Washindi Ulaya(1): 1982-83.
Super Cup ya Ulaya (1): 1983.Ferguson cradles the FA Cup in 1990. He would get his hands on many more trophies...
Ferguson kisses the European Cup-Winners' Cup after victory in 1991
Eric Cantona (right) was possibly Ferguson's most important acquisition
MANCHESTER UNITED
Ligi Kuu England (13): 1992-93, 1993-94, 1995-96, 1996-97, 1998-99, 1999-2000, 2000-01, 2002-03, 2006-07, 2007-08, 2008-09, 2010-11, 2012-13.
Kombe la FA (5): 1989-90, 1993-94, 1995-96, 1998-99, 2003-04.
Kombe la Ligi Cup (4): 1991-92, 2005-06, 2008-09, 2009-10.
Ngao ya Jamii/Hisani (10): 1990 (shared), 1993, 1994, 1996, 1997, 2003, 2007, 2008, 2010, 2011.
Ligi ya Mabingwa Ulaya (2): 1998-99, 2007-08.
Kombe la Washindi Ulaya (1): 1990-91.
Super Cup ya Ulaya(1): 1991.
Kombe la Mabara(1): 1999.
Klabu Bingwa ya Dunia (1): 2008.


Ferguson watches his first United game, a defeat by Oxford in 1986
Kocha huyo mwenye umri wa miaka 71 anajiandaa kuaga umati wa mashabiki Uwanja wa Old Trafford Jumapili baada ya mechi ya United dhidi ya Swansea, wakati watakapokabidhiwa taji la ubingwa wa Ligi Kuu England, hilo likiwa la 13 chini ya Ferguson.
Mazungumzo yanaendelea kumsaka mrithi wake na kocha wa Everton, David Moyes ni miongoni mwa wanaopewa nafasi. 

No comments:

Post a Comment