Pages

Thursday, May 9, 2013

CRISTIANO RONALDO APANDIWA NDEGE NA DAVID GILL SPAIN.


Christiano Ronaldo akiwa ameshika Kombe enzi akiichezea Manchester United.
Mtendaji mkuu wa klabu ya Man Utd David Gill ameshindwa kuficha hisia na kuamua kumpandia ndege kwenda kuzungumza na Ajenti wake huko Hispania juu ya mshambuliaji kutoka nchini Ureno Cristiano Ronaldo ambaye bado anaendelea kuhusishwa na mpango wa kurejea old Trafford.

David Gill ameshindwa kuficha hisia za kumuona mshambuliaji huyo akirejea katika himaya ya Mashtamni wekundu, alipohojiwa na kituo cha televisheni cha Sky Sports ambapo amesema si vibaya endapo ronaldo atarejea katika utawala wao. 

Amesema Cristiano Ronaldo ni mchezaji mzuri na mwenye hadhi ya kuitumikia klabu ya Man Utd ambayo ilimuuza mwaka 2009, baada ya kuonyesha uwezo mzuri ambao uliwavutia Real Madrid na kukubalia kutoa kiasi cha paund million 80 kama adayake ya uhamisho. 

Gill amesema hatoshangazwa na mpango wa Ronaldo endapo utatua mezani kwake kwa ajili ya kusajiliwa kwa mara nyingine tena, hivyo amesisitiza suala hilo kuachwa na kuamini bado mshambuliaji huyo ni bora kati ya wachezaji walio bora. 

No comments:

Post a Comment