Pages

Monday, May 20, 2013

RIADHA WAJIPANGA KUCHAGUA TIMU YA TAIFA YA VIJANA












MASHINDANO ya Wazi ya Mchezo wa Riadha, yanatarajia kuendelea kutimua vumbi Mei 25 mkoani Dodoma baada ya kufanyika wiki iliyopita mkoani Arusha na jijiji Dar es Salaam.


Mashindano hayo ndio yatakua ya mwisho na kuwapa nafasi viongozi wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) kuchagua timu ya taifa ya vijana ambayo itaiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Afrika Mashariki.

Akizungumza jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Chama cha Riadha Tanzania (RT), Suleiman Nyambui alisema hayo ni mwendelezo wa mashindano yaliyofanyika wiki iliyopita ambayo yaliudhuriwa na klabu mbalimbali.

“Lengo la mashindano hayo ni kutafuta vijana chini ya miaka 20 kwa ajili ya kuunda timu ya Taifa ya viijana,” alisema Nyambui.
Alisema baada ya kumalizika kwa mashindano hayo, kamati itakaa ili kuorodhesha majina ya vijana watakaoweza kuunda timu ya taifa ya vijana chini ya miaka 20.

Alisema anawaomba wapenzi wa mchezo huo kujitokeza kwa wingi kwa ajili ya kuonesha ushirikiano kwa wachezaji watakaojitokeza kushiriki katika mashindano hayo.

No comments:

Post a Comment