Pages

Monday, May 20, 2013

CBE YAIVUA UBINGWA WA POOLTABLE IFM



CHUO Kikuu cha Biashara (CBE) jana kimetawazwa kuwa mabingwa wa mchezo wa Pool Table mkoa wa Dar es Salaam baada ya kukivua ubingwa Chuo Kikuu cha Usimamizi wa Fedha (IFM)  kwenye mashindano ya Pool Table kwa Vyuo Vikuu vya Dar es salaam.

CBE ambayo imeingia fainali mara tatu mfululizo  na kutolewa na IFM walionekana kupania mchezo huo baada ya kuwaondoa mabingwa hao watetezi kwa mabao 13 kwa 4 kwenye fainali zilizofanyika kwenye baa ya Meeda iliyopo Sinza, Kinondoni.

Baada ya CBE kuifunga IFM, walizawadiwa shilingi laki 500,000 na watawakilisha mkoa wa Dar es Salaam kwenye fainali za Pool Table zitakazofanyika baadae hapa jijini Dar es Salaam na mshindi wa pili alizawadiwa 300,000.

Akizungumza na baada ya mchezo kumalizika , nahodha wa IFM Patrick Peter alisema kweli wamesitikitishwa na kitendo cha kuvuliwa ubingwa ila kwenye ushindani lazima mmoja apatikane tunakubali matokeo.
“Kwenye mchezo wowote mshindi ni mmoja na sisi tunakubali tumevuliwa ubingwa kwa sababu wenzetu wametuzidi tunawatakia kila la heri”, alisema Peter

Kwa mshindi mmoja moja Patrick Peter wa IFM alimfunga Salehe Amin wa Chuo cha IAMCO na kuondoka na zawadi ya shilingi 150,000 pia atawakilisha Dar es Salaam kwenye fainali za Taifa za mchezaji mmoja mmoja.

Pia kulikuwepo burudani ya Joh Makini aka mwamba wa Kaskazini ambaye alitoa burudani ya kufa mtu na kuwapagawisha wanavyuo
Timu ya CBE wakishangilia baada ya kupokea 500,000 taslimu baada ya kuivua ubingwa IFM

Meneja wa bia ya Safari, Oscar Shelukindo akimkabidhi fedha taslimu 150,000 mchezaji Patrick Peter wa IFM  baada ya kushinda kwenye mchezo wa mchezaji mmoja moja

CBE wakishangilia baada ya kutwaa ubingwa wa Mkoa wa Dar es Salaam

Patrick Peter wa IFM akicheza pool table

John Makini akitoa burudani

No comments:

Post a Comment