Pages

Friday, May 17, 2013

REDSS MISS MOSHI KUPATIKANA KESHO AVENTURE

Baadhi ya Redd Miss Moshi

FAINALI za kumsaka Redds Miss Moshi 2013 itakayofanyika kesho, mwaka huu katika ukumbi wa Aventure uliopo Moshi

Akizungumza kwa njia ya simu, mratibu wa mashindano hayo,  Moses Komba alisema kuwa jumla ya walibwende wapatao 19 watachuana kumsaka malkia wa Moshi.

Moses alisema tayari mchujo wa kwanza umeshafanyika ambapo warembo wote waliingia kambini kujifua na kuongeza kwamba mashindano ya mwaka ambayo ni ya pili tangu yaanzishwe yatakuwa ni ya aina yake.

“Maandalizi yamekamilika na warembo wote wapo kambini katika ukumbi wa Aventure na tunategemea wadau watashuhudia kitu tofauti katika shindano la mwaka huu,” alisema Komba.
Pia alisema viingilio katika mashindano ya mwaka huu,  viti vya dhahabu viingilio vitakuwa sh. 50,000, viti vya V.I.P vitakuwa ni sh. 30,000 na viingilio vya kawaida ni sh. 15,000.

Wadhmini wengine na Redds, Panone, Baba G na Zoom Net Printers ambapo kwa upande wa burudani alisema atakuwepo msanii mkongwe wa kizazi kipya Dully Sykes akisindikizwa na wasanii wengine kutoka Moshi.

No comments:

Post a Comment