Pages

Friday, May 17, 2013

RAFAEL BENITEZ KUONDOKA CHELSEA KWA TABASAMU



Rafael Banitez na kombe la Ligi ya Uropa baada ya Chelsea kufunga Benfica juzi.

Hatimae meneja Rafael Benitez ataondoka Chelsea akiwa na tabasamu baada ya timu yake kubeba ubingwa wa Kombe la Europa League kwa kuifunga timu ya Benfica ya Ureno 2-1 usiku wa Jumatano katika uwanja wa Amsterdam, Uholanzi. 

Hii ni baada ya Branislav Ivanovic kufunga bao maridadi kwa kichwa wakati wa muda wa ziada wa majeruhi.
Tangu alipoingia Chelsea kama kaimu mkufunzi Benitez amekuwa na wakati mgumu kwani mashabiki wa Old Trafford wamekuwa hawampendi. 

Lakini baada ya kuifunga Benfica mashabiki hao hao ambao walikuwa hawampendi Benitez waliishangilia ushindi wa timu yao kwa vifijo na nderemo huku wakisahau chuki waliokuwa nao kwa kaimu meneja huyo. 
Mwaka jana Chelesea ilishinda Kombe la Klabu bingwa bara Ulaya na mwaka huu wamebeba kombe la Europa League.
Bao lakwanza la Chelsea lilifungwa na mshambulizi Fernando Torres nao Benfica wakapata lao kupitia mwaju wa penalti uliofungwa na Oscar Cardozo.


Ushindi wa Chelsea unamfanya Rafael Benitez kuwa meneja wa nne kushinda kombe la Klabu Bingwa Uropa na la Europa League zaidi ya mara mmoja. 

Wengine amabo wamewahi kushinda kumbe hilo zaidi ya mara moja niGiovanni Trapattoni: 1977 (Juventus); 1991 (Inter); 1993 (Juventus) ,Luis Molowny: 1985 & 1986 (Real Madrid) Juande Ramos: 2006 & 2007 (Sevilla).

No comments:

Post a Comment