Pages

Friday, May 17, 2013

JULIANA KANYOMOZI AKANA NDOA NA JAJI IAN WA TUSKER PROJECT FAME



Majaji wa shindano la Tusker Project Fame, Ian Mbugua kushoto, Juliana Kanyomonzi, na Hermes Bariki wakiwa katika picha ya pamoja wakati wa kinyang'anyiro hicho
KAMPALA, Uganda
“Sijawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Ian. Yeye ni mmoja wa watu ninaofanya nao kazi pamoja Tusker Project Fame (TPF) na sio zaidi ya hapo. Namuheshimu yeye kama jaji mwenza na mtu wa familia. Tetesi hizi ni upotoshaji tu”
MKALI wa muziki Afrika Mashariki na Kati, Juliana Kanyomozi waUganda, jana amezikana taarifa zilizozagaa kupitia mitandao ya kijamii, kuwa anajiandaa kufunga pingu za maisha na Ian Mbugua - Jaji mwenza wa shindano la Tusker Project Fame.
Kanyomozi (picha ndogo kulia), ametumia ukurasa wake wa Facebook kuzikana taarifa zilizodaiwa kutoka kwa rafiki wa karibu wa Jaji Ian, ambaye ni mume wa mtu, akimkariri jaji huyo kuwa amezama kimahusiano na anatarajia kufunga ndoa baadaye mwaka huu.
“Habari zenu marafiki, nimeona tetesi kupitia mitandao hii ya kijamii ikisema mengi kunihusu mimi na nimeona nivunje ukimya juu ya hilo kwa kusema kwamba sina mpango wowote wa kufunga ndoa na Jaji Ian.
“Sijawahi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na Ian. Yeye ni mmoja wa watu ninaofanya nao kazi pamoja Tusker Project Fame (TPF) na sio zaidi ya hapo. Namuheshimu yeye kama jaji mwenza na mtu wa familia. Tetesi hizi ni upotoshaji tu,” aliandika Kanyomozi.
Mapema Jumamosi iliyopita, mitandao ya kijamii ya nchini Uganda ilimkariri mtu aliyejiita rafiki wa karibu wa Jaji Ian akithibitisha kuwa rafikiye huyo hafichi mahusiano yake na Juliana na kuwa wanajipanga kufunga ndoa.
Chanzo hicho kilimkariri Jaji Ian akisema kuwa: “Siwezi kuitoa sadaka furaha yangu, Juliana ndiye furaha yangu. Hata kama itanigharimu kuchukiwa na kila mmoja, niko tayari kumuoa Juliana. Yeye ndiye Juliet wangu, na mimi ndiye Romeo wake."

No comments:

Post a Comment