Pages

Friday, May 31, 2013

MOYES ANATEMBEA NA MAJINA MATATU MFUKONI

 
KOCHA mpya wa Manchester United, David Moyes, sasa anatembea na majina matatu ya viungo, ambao mmojawapo atamsajili katika usajili wa majira haya ya joto.

Gazeti la "The Daily Mail", limeeleza kuwa nyota wa Barcelona, Cesc Fabregas, ni mmoja kati ya viungo anaotaka kuwasajili.

Moyes pia katika orodha yake mbali na Fabregas, anamhitaji mchezaji mweza wa Barcelona, Thiago Alcantara na nyota wa PSV Eindhoven, Kevin Strootman.


No comments:

Post a Comment