Pages

Friday, May 31, 2013

'HATA KWA EURO 1,000 RONALDO HAUZWI'

 
RAIS wa Real Madrid, Florentino Perez, kwa mara nyingine amesema kwamba hataki kabisa kumuuza Cristiano Ronaldo, ambaye bado anahusishwa na kutua Manchester United na PSG.

Perez alifafanua: "Nitafanya kila liwezekanalo kwa nguvu zangu ili kumpa mkataba mpya. Amebakiza miaka miwili katika mkataba wake, ni mchezaji bora duniani na ataiboresha timu yetu, yeye ni kama kiongozi.

"Sitamuuza hata kwa Euro milioni 1,000, hii si klabu ya kufanya mauzo. Ningependa awepo hapa hadi atakapotundika daluga, itakuwa ni vema kabisa."

No comments:

Post a Comment