Pages

Wednesday, May 15, 2013

LOIC REMY WA QUEENS PARK RANGERS ASHIKILIWA NA POLISI KWA TUHUMA ZA UBAKAJI


Mshambuliaji Queens Park Rangers Loic Remy amekamatwa kwa makosa ya ubakaji  na wenzake wawili.

Mshambuliaji huyo mwenye miaka 26 ambaye pia ni mchezaji wa kimataifa wa Ufaransa anashikiliwa na askari wa uchunguzi wa Scotland Yard's wa kitengo cha makosa ya ubakaji akiwa pamoja na vijana wenzake wawili ambao walikamatwa huko Fulham, Magharibi mwa London .

Vijana hao wanashikiliwa kwa mahojiano zaidi baada ya kumuingilia mwanamama mwenye miaka  34 ambaye alibakwa  siku ya jumatatu  na mashitaka hayo yalipitiwa na  Met kutoka Askari wa  Kent  jumatatu iliyopita.

Msemaji wa  Metropolitan Polisi amesema : "watu watatu wenye umri kati, miaka  26, 23 na 22, walikamtwa  katika kitongoji cha  Fulham kwa makosa ya ubakaji na bado watabakia katika kituo cha polisi hapa  London ".

No comments:

Post a Comment