London:
BAADA ya kuweka rekodi mpya ya ufungaji Chelsea, Frank Lampard ameitoa rekodi
hiyo kwa Marehemu Mama yake, wachezaji wenzake na Mashabiki wa klabu hiyo.
Mabao mawili
aliyoyafunga kwenye ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Aston Villa, yamemfanya
Lampard kufikisha jumla ya mabao 203 na kuvunja rekodi ya Bobby Tambling
aliyekuwa na mabao 202.
@@@@
Alonso: Sisi
tunachonga tu
Madrid: XABI
Alonso amekanusha taarifa kwamba wachezaji wa Real Madrid wameamuriwa
kutokuzungumza na vyombo vya habari, baada ya Pepe kutoa maneno makali dhidi ya
Jose Mourinho.
“Kila mtu
anaweza kuzungumza anachokitaka na hakuna kitu cha kuogopa, hakuna mtu
anayetuambia nini cha kusema,” alisema Alonso baada ya sare ya 1-1 dhidi ya
Espanyol, juzi.
@@@
Adebayor
apania kuiua Arsenal
London:
MSHAMBULIAJI wa Tottenham Hotspur, Emmanuel Adebayor (29) ameweka wazi kuwa
anatamani kuua ndoto za Arsenal kumaliza kwanye ‘Big 4’ msimu huu.
“Akili yangu
yote iko Tottenham, sijali kitakachowakuta Arsenal, kama ikibidi niwaue itabidi
nifanye hivyo kwa sababu mchezo huu unahitaji ufanye vizuri kwenye timu yako,”
alisema Adebayor.
@@@@
Buffon: Tunakazi
kuikamata Bayern
TURIN: Italia
LICHA ya Juventus
kuchukua ubingwa wa pili mfululizo wa Serie A, nahodha wa timu hiyo Gianluigi
Buffon amekiri kuwa Bianconeri wanahitaji kufanya kazi kubwa kama wanataka
kufanya vizuri Ulaya.
Buffon anaamini kwamba,
kwa sasa Bayern Munich wako hatua mbili mbele ya timu zote barani Ulaya, na
wataendelea kutesa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Juventus walikutana na
kipigo cha jumla cha mabao 4-0, kutoka kwa Bayern, kwenye robo fainali, kabla
ya Wajerumani hao, kupata ushindi wa jumla wa mabao 7-0 dhidi ya Barcelona
kwenye nusu fainali.
Pamoja na kutawala soka
la Italia, Buffon anaamini kuwa Juve bado wanamtihani mkubwa kama wanataka
kuchukua Ligi ya Mabingwa Ulaya.
“Kuchukua
ligi ya mabingwa, sisi pamoja na klabu zote Ulaya zinatakiwa kujipanga ili
kuifikia Bayern Munich, ambayo iko
No comments:
Post a Comment