Pages

Wednesday, May 22, 2013

KOCHA MPYA DAVID MAOYES ATUA MANCHESTER UNITED KWA MARA YA KWANZA TAYARI KWA KAZI MSIMU HUU UNAOKUJA!!! AFATANA NA BABU SIR ALEX FERGUSON


DAVID MOYES ameanza himaya yake kwa Mabingwa wa England Manchester United tangu kustaafu Sir Alex Ferguson wakati alipokwenda Carrington, Kituo cha Mazoezi cha Mabingwa hao, kwa mara ya kwanza kukutana na Wachezaji na Wafanyakazi wote.

Ingawa anatakiwa kuanza kazi rasmi hapo Julai 1, Moyes ameamua kuanza mapema ili kurahisisha Kipindi hiki cha Mpito ambacho Man United inashuhudia mabadiliko ya Uongozi kwa mara ya kwanza tangu Mwaka 1986 Sir Alex Ferguson alipotwaa madaraka..

Akiongea Jana mara baada ya Mechi yake ya mwisho akiwa na Everton walipofungwa 2-1 na Chelsea, Moyes alisema: “Nadhani kwa Wiki mbili zijazo ntakuwa na kazi mbili. Ntakuwa pia Siku nyingine nakwenda Finch Park [Kituo cha Mazoezi cha Everton] kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa kwa Meneja mpya.”

Moyes, ambae alidumu Everton Miaka 11, anarithi himaya ya Sir Alex Ferguson ya mafanikio makubwa ya kutwaa Vikombe 38 katika Miaka 26 yakiwemo Mataji ya Ubingwa wa Ligi Kuu England mara 13.

Kazi kubwa ambayo itabidi aanze nayo ni kuamua hatima ya Straika Wayne Rooney ambae Sir Alex Ferguson alitoboa hivi karibuni kuwa ameomba kuihama Man United.

Hii ni mara ya Pili ndani ya Miaka mitatu kwa Rooney kuomba Uhamisho na hili itabidi litafutiwe ufumbuzi na Moyes ambae ndie Mtu aliemkuza Rooney alipokuwa Everton na kumpandisha kucheza Timu ya Kwanza akiwa na Miaka 16 tu.

Lakini, Rooney alikorofishana na Moyes mara baada ya kuihama Everton na kwenda Man United wakati Straika huyo alipoandika kwenye Kitabu chake kashfa dhidi ya Moyes ambae alishitaki na kushinda Kesi na kulipwa Fidia.

Hata hivyo, Mwaka 2010, Rooney alimtaka radhi Moyes ambae alimsamehe wakati huo huo.

Hata hivyo Wachambuzi wanahisi kuondoka kwa Rooney wakati huu hakutazua athari yeyote kwa Mabingwa Man United kwani wanae Mfungaji Bora wa England, Robin Van Persie, aliefunga Bao 26 katika Msimu wake wa kwanza na Man United na kutwaa Buti ya Dhahabu.

Pia, Moyes anatarajiwa kuamua hatima za Wasaidizi wa Ferguson, Makocha Mike Phelan na Rene Meulensteen, ingawa mwenyewe ameshadokeza hakutakuwa na mabadiliko makubwa lakini inaaminika aliekuwa Msaidizi wa Moyes huko Everton, Steve Round, Kocha Jimmy Lumsden na Mchezaji wa zamani wa Man United, Phil Neville, watakuwa nae kwenye Benchi la Ufundi la Mabingwa hao.

No comments:

Post a Comment