Pages

Tuesday, May 28, 2013

KIBADENI AANZA KAZI SIMBA, JULIO, MATOLA, AMRI SAID NDANI YA NYUMBA

Kibadeni, Julio na Saleh Ally wakizungumza leo asubuhi kwenye Uwanja wa Kinesi, Dar.


Kocha Mkuu wa Simba, Abddallah KIbadeni ‘King Mputa’ ameanza kazi leo rasmi.
Kibadeni ameanza kazi ya kuinoa Simba, lakini kwa kusimamia zoezi la mchujo wa wachezaji wapya lililofanyika kwenye Uwanja wa Kinesi jijini Dar.
Matola na bosi wake mpya, Kibadeni.

KIbadeni alishirikiana na msaidizi wake, Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ lakini pia makocha wa timu za vijana na watoto, Selemani Matola, Amri Saidi pamoja na Patrick Rweyemamu.
Benchi la ufundi la Simba na Katibu Mkuu, Evodius Mtawala

Kibadeni, mmoja wa makocha wakongwe na hodari nchini, ameiambia Salehjembe kwamba ameishamalizana na Simba kwa kusaini mkataba wa miezi miwili.
Kijana akisali kabla ya kuanza majaribio kuwania kucheza Simba...
“Kweli nimemalizana na Simba, tumeingia mkataba wa miezi miwili na kazi inaanza sasa,” alisema.
Vijana waliofika kuwania kucheza Simba

“Kikubwa watuamini na kazi tutaifanya vizuri kwa kuwa hakuna sababu ya kuwa na hofu.”
KIbadeni anachukua nafasi ya Patrick Liewig ambaye yuko kwa Ufaransa na ameshaeleza wazi haelewi kutimuliwa kwake.
 


Vijana wanaowania kucheza Simba...
Julio, Matola wakifuatilia vijana wanaowania kucheza Simba.   
   Kwa hisani ya  Salehjembe.blogspot.com   
                                                              

No comments:

Post a Comment