Pages

Tuesday, May 28, 2013

BARCELONA WAANZA KUUZA JEZI YA NEYMAR

  
Barcelona ni noma, amini usiamini! Siku mbili baada ya kumsajili Neymar wa Brazil, tayari  wameshaanza kuuza jezi zake.

Kuonyesha timu za Ulaya zinajua biashara, jezi za Neymar, mgongoni zikiwa na namba 11 zimeshaingia sokoni na zinanunuliwa kwa kasi kubwa.
Awali jezi hiyo ilikuwa inavaliwa na Thiago Alcantara lakini sasa amekabidhiwa Mbrazil huyo ambaye usajili wake ndiyo gumzo zaidi kwa La Liga, msimu huu.

Barcelona tayari ‘imefunga naye ndoa’ kwa miaka mitano na anatarajiwa hivi karibuni kutua na kuanza kazi na klabu yake hiyo mpya.
Mashabiki wa Barcelona walionekana kuwa na furaha kumpata mshambuliaji huyo wa Santos ambaye ndiye maarufu zaidi nchini Brazil kwa kipindi hiki.

No comments:

Post a Comment