Pages

Sunday, May 19, 2013

DAVID BECKHAM AAGWAA KWA USHINDI PARIS, ABUBUJIKWA MACHOZI



DAVID BECKHAM alitoka Uwanjani katika Mechi yake ya mwisho ya Nyumbani ya Klabu yake Paris St-Germain ambayo huenda ikawa ndio ya mwisho katika maisha yake ya Soka ya Miaka 20 huku akibubujikwa machozi.
Beckham, ambae alianza Mechi hiyo ya Ligi dhidi ya Brest kama Nahodha, alibadilishwa katika Dakika ya 81 na Mechi kusimama kwa muda huku Wachezaji wenzake wa PSG wakimshangilia nay eye akawa akitoka nje kwa machozi.

Mashabiki wengi wa PSG wamekuwa wakililia Beckham, Miaka 38, abakie kama Mchezaji badala ya kustaafu.
Msimu huu PSG ndio wamekuwa Mabingwa wa France na bado wana Mechi moja ya Ligi Jumapili ijayo watakayocheza Ugenini na Lorient lakini inaaminika Beckham hatakuwepo.

Katika Mechi ya Jana PSG waliifunga Brest Bao 3-1 huku Beckham akitengeneza Bao moja kwa Kona yake kuunganishwa na Blaise Matuidi na Bao nyingine mbili kufungwa na Zlatan Ibrahimovic.
Bao la Brest lilifungwa na Charlison Benschop.

Mara baada ya Filimbi ya mwisho kwenye Mechi hiyo na Brest, Beckham aliwahutubia Mashabiki na kusema: “Nataka kumshukuru kila Mtu hapa Paris-Wachezaji wenzangu, Wafanyakazi na Mashabiki. Ni kitu kikubwa kumalizia Soka langu hapa. Nimemaliza Soka nikiwa Bingwa na kwenye Timu iliyonifanya nijione kama nimekaa Miaka 10!”

Wachezaji wa PSG walimbeba na kumrusharusha juu huku akishuhudia na Mkewe Victoria na Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy.


Wachezaji wa PSG wakimpongeza David Beckham wakati anapumzika


Beckham na Ibrahimovic wakiagana

Beckham

Beckham akitupa mkono juu

Victoria Beckham akiingia uwanjani kumwangalia mumewe wakati wa mechi ya mwisho

Beckham akiendesha mpira uwanjani

wachezaji wakipongezana

Bosi nae Carlo Ancelotti akiteta na Beckham huku akitoka uwanjani

Mke wake Victoria na mtoto DAVID BECKHAM
Baada ya kuwika katika Soka kwa Miaka 20, David Beckham, Miaka 38, Alhamisi Mei 16 ametangaza kustaafu Soka mwishoni mwa Msimu huu.
Winners: United came from a goal down to snatch the win over Bayern Munich in Barcelona Beckham, Nahodha wa zamani wa England aliyoichezea mara 115, akiwa na Mabingwa wa England, Manchester United, aliweza kutwaa Ubingwa wa Ligi Kuu England mara 6 pamoja na UEFA CHAMPIONZ LIGI.
Mwezi Januari, Beckham alisaini Mkataba wa kuichezea Paris St-Germain ya France kwa Miezi mitano.
PSG wamebakiza Mechi 2 Msimu huu, ile ya Nyumbani dhidi ya Brest Jumamosi hii na Ugenini na Lorient hapo Mei 26.


KUHUSU BECKHAM
-1992-2003: Manchester United (Mechi 356, Magoli 85)
-1994-1995: Preston North End (Mkopo) (Mechi 5, Goli 2)
-2003-2007: Real Madrid (Mechi 157, Magoli 19)
-2007-2012: Los Angeles Galaxy (Mechi 118, Magoli 20)
-2009-2010: Mkopo AC Milan (Mechi 33, Magoli 2)
-2013: Paris St-Germain (Mechi 13)


Beckham, ambae Mshahara wake akiwa na PSG huenda kwenye Mifuko ya Hisani ya kusaidiaWatoto, ameichezea PSG Mechi 13 tangu ahamie hapo.
Akiwa na Klabu za Man United, Real Madrid, Los Angeles Galaxy, AC Milan na PSG, amefanikiwa kutwaa Makombe 19 na Ubingwa wa Ligi za Nchi mara 10.
Beckham ametamka: “Ungeniambia nilipokuwa Mtoto kuwa ningechezea na kutwaa Mataji na Klabu niliyoipenda ya Manchested United, kuwa Nahodha wa Nchi yangu kwa fahari kubwa na kuichezea zaidi ya mara 100 na kuzichezea Klabu kubwa Duniani, ningekwambia hiyo ni ndoto!”
Aliongeza: “Nimebahatika kutimiza Ndoto hiyo!”

Beckham, aliezaliwa Mei 2, 1975, alijiunga na Man United Mwaka 1991 akiwa Mcheza Soka Mwanafunzi na kuanza kuichezea Timu ya Kwanza Mwaka 1992 na kusaini Mkataba wake wa kwanza wa Mchezaji wa Kulipwa Mwaka 1993.
Akiwa Old Trafford, Beckham alijijengea Jina kubwa Duniani kote na umaarufu wake kuongezeka pale alipomuoa Mwimbaji maarufu wa Kundi la Spice Girls, Victoria Adams.
Mwaka 2003 Beckham aliihama Man United na kwenda Spain kuichezea Real Madrid ambako alifanikiwa kutwaa Taji la La Liga Mwaka 2007 na kisha kuhamia Marekani kuichezea LA Galaxy.
Akiwa na LA Galaxy, mara mbili, Mwaka 2009 na 2010, Beckham alicheza kwa Mkopo huko Italy na Klabu ya AC Milan.

Beckham alianza kuichezea England kwenye Mechi na Moldova Mwaka 1996 na kuwa Nahodha wake kuanzia 2000 hadi 2006 na kucheza Mechi yake ya 115 na ya mwisho dhidi ya Belarus Mwaka 2009.
Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron, amesema: “Ni Mchezaji Bora katika maisha yake. Si hilo tu, ni Balozi Bora kwa Nchi yake!”
Nae Meneja wa England Roy Hodgson alitamka: "Maisha yake ya Soka yaling’ara, ni Nguli na namtakia maisha mema ya baadae!"

No comments:

Post a Comment