Pages

Friday, May 31, 2013

CHELSEA YAZUNGUMZA NA DE ROSSI


Chelsea ipo katika mazungumza na Kiungo wa AS Roma, Daniele de Rossi, ikihitaji kummiliki kuelekea usajili wa majira haya ya joto.

Taarifa zimeeleza kuwa, Jose Mourinho amempendekeza De Rossi kwamba anastahili kufanya naye kazi wakati huu ambao anajiandaa kuiongoza Chelsea.

De Rossi alisaini mkataba mpya wa kuitumikia Roma msimu uliopita, lakini si mwenye furaha, baada ya kukosa namba katika kikosi cha kwanza, huku pia uhusiano wake na mashabiki wa timu hiyo ukivunjika.

 @@@@@@@@@@@

Iago Aspas kuitembelea Liverpool

Liverpool imelenga kumsajili Mshambuliaji wa Celta Vigo, Iago Aspas na zoezi hilo huenda likakamilika wiki ijayo.

Gazeti la "The Daily Mail", limeeleza kuwa Liverpool imekubali kutoa ada ya uhamisho ambayo inaaminika kuwa pauni milioni sita, ili kuweza kumsajili Aspas, 25
@@@@@@@@@

Julio Cesar ahusishwa Arsenal

KIPA wa Queens Park Rangers ambayo imeshuka daraja, Julio Cesar, ameweka bayana kwamba tayari amefanya mazungumzo na Klabu moja ya Ligi Kuu England, ambapo wengi wanatabiri kwamba huenda ikawa ni Arsenal.

Cesar ataruhusiwa kuondoka QPR kwa bei rahisi na kwamba inaaminika kuwa kwa pauni 70,000 kwa wiki anazohitaji, tayari Arsenal imezungumza naye ili kuipata huduma yake wakati huu ambao inasaka kipa mpya.

Kipa huyo wa Kimataifa wa Brazil ambaye anajiandaa kuivaa England Jumapili katika mechi ya kimataifa ya kirafiki itakayopigwa Rio de Janeiro, alisema: “Tayari nimezungumza na klabu nyingine za England na kutoka nchi nyingine, lakini hakuna lolote limeshafikiwa."

No comments:

Post a Comment