Pages

Sunday, May 12, 2013

CHARLES BABA WA MASHUJAA AMTAMBULISHA MCHUMBA WAKE KWA MASHABIKI WAKATI WA UZINDUZI WA ALBAMU YA RISASI KIDOLE

Wacheza shoo wa Mashujaa wakiwa kazini

Add caption







Charles Baba akiwa amepiga amechuchumaa wakati akimvika pete ya uchumba Rehema Sospeter 



BENDI ya Mashujaa jana   usiku ilikata kiu ya mashabiki wa muziki wa dansi baada ya kutoa burudani iliyo konga nyoyo za wadau kwenye ukumbi wa Business Park, Kijitonyama, jijini Dar es Salaam.

Mashujaa walikuwa wanatambulisha albamu yao ya Risasi Kidole kwa mashabiki wao walisindikizwa na FM Academia bendi chini ya rais wao Nyoshi el Sadaat pia walitoa burudani nzuri.

Kwenye onyesho hilo FM Academia ndio walikuwa wa kwanza kupanda jukwaani na kutoa burudani nzuri na wakafuatiwa na Mashujaa ambao nao walitoa burudani ya nguvu bila kusimama.
Mashabiki walionekana kufurahia dansi kwani muda wote walikuwa wamesimama wakicheza na kuwatunza wacheza shoo na waimbaji.

Mkurugenzi wa Mashujaa Bendi, Sakina Mohmed Mbange maarufu kama Mama Sakina hakuwa nyuma kuonyesha furaha yake kwani alikuwa anacheza muda wote huku akifurahi hadi kutokwa na machozi.

Rais wa bendi ya Mashujaa, Charles Baba alimtambulisha mpenzi wake Rehema Sospeter kwa mashabiki na kumvisha pete ya uchumba na kusema ndie mke wake mtarajiwa na sasa wapo kwenye maandalizi ya kufunga ndoa. 

No comments:

Post a Comment